Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tshishimbi: Hatukutarajia sare

NAHODHA wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi amesema mipango ya timu yao ilikuwa ni ushindi na si matokeo ya sare ambayo wameyapata.
Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Kariobang Sharks katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Mwananchi kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Tshishimbi amesema mipango yao haikuwa sare au kupoteza mechi hiyo.
"Tulijipanga kwa ushindi, lakini bahati haikuwa upande wetu, pamoja na matokeo ya sare, bado timu iko vizuri,".
Nahodha Kariobang Sharks, Erick Juma alisema Yanga imecheza kwa kiwango bora japo ameeleza kwamba tofauti na walivyofahamu timu hiyo, msimu huu imekuwa na nyota wengi wa kimataifa ambao wamecheza kikosi cha kwanza.