Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA yashikilia hatma KMC Ligi Kuu

Muktasari:

  • Katika mechi hizo tatu zitakazopigwa leo, Fountain Gate itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, huku Coastal Union ya mjini Tanga ikiwa Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Namungo FC. Kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam, ambapo wenyeji KMC FC ikiwa itapoteza dhidi ya TRA United, saa 2:OO Usiku.

BAADA ya kupisha Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa la FIFA kwa wiki mbili, Ligi Kuu Bara inaendelea tena leo kwa mechi tatu kupigwa kwenye viwanja mbalimbali, huku hatma ya KMC FC kushuka daraja ikiwa mikononi kwa TRA United.

Katika mechi hizo tatu zitakazopigwa leo, Fountain Gate itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, huku Coastal Union ya mjini Tanga ikiwa Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Namungo FC. Kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam, ambapo wenyeji KMC FC ikiwa itapoteza dhidi ya TRA United, saa 2:OO Usiku.


KMC FC v TRA UNITED

Baada ya kushuhudia Geita Gold na Kagera Sugar zikijihakikishia nafasi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao, huenda leo tukaishuhudia KMC ikiwa timu ya kwanza kushuka daraja ikitoka Ligi Kuu, kama itapoteza dhidi ya TRA United.

KMC inaingia ikiwa na mwenendo usioridhisha hadi sasa, imeshinda mechi mbili tu, sare tatu na kupoteza 20, kati ya 25.

KMC inaburuza mkiani akiwa nafasi ya 16 na pointi tisa, ikipoteza mechi ya leo itashuka daraja kwa sababu timu zinazoshuka moja kwa moja ni mbili, hivyo, hata ikishinda pia mechi nne zilizobakia itafikisha pointi 21, ambazo ni moja pungufu ya Mbeya City iliyopo nafasi ya 14 na pointi 22..

TRA United inaingia katika mechi hiyo ikitoka kuchapwa mabao 2-1, na Fountain Gate. Wanahitaji ushindi ili kujisogeza katika nafas ya tano inayoshikwa na JKT Tanzania na pointi 38.


WASIKIE MAKOCHA

Kaimu Kocha Mkuu wa KMC FC, Imani Mwalupetelo alisema licha ya presha kubwa inayokabiliana na kikosi hicho.

“Tumepata nafasi ya kurekebisha changamoto tulizonazo kuanzia eneo la kujilinda hadi la ushambuliaji, tunatambua nafasi tuliyopo sio nzuri ila hatupaswi kucheza kwa woga wowote tunakutana na timu bora,” alisema Imani.

Naye Kocha Mkuu wa TRA United, Mrundi Etienne Ndayiragije alisema licha ya kucheza na timu yenye mwenendo mbaya hadi sasa, ila hawatacheza kwa kuwadharau, kwani malengo yao ni kupata pointi tatu baada ya kupoteza mechi ya mwisho.


FOUNTAIN v AZAM FC

Timu zote zinaingia zikiwa na morali baada ya kushinda mechi zao za mwisho, ambapo Fountain Gate iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya TRA United, huku Azam FC kikiwa na kumbukumbu ya kuifunga KMC FC mabao 3-0.

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa raundi ya 16, bora ya Michuano ya Kombe la CRDB, Aprili 12, 2026, ambapo Azam FC ilishinda mabao 4-0, japo kwenye mechi ya Ligi Kuu mzunguko wa kwanza zilitoka suluhu, Januari 20, 2026.


COASTAL v NAMUNGO FC

Mechi nyingine inayosubiriwa kwa hamu ni ya Coastal Union dhidi ya Namungo FC inayopita katika kipindi kigumu cha kukosa ushindi katika mechi 15 za Ligi Kuu.

Coastal Union chini ya Kocha, Fikiri Elias inaingia ikiwa na kumbukumbu nzuri baada ya mechi ya mwisho kuifunga Mashujaa FC bao 1-0, huku Namungo mara ya mwisho kushinda ilikuwa Januari 31, 2026 dhidi ya KMC.

Mechi hii ni ya kisasi kwa Coastal Union, kwa sababu raundi ya kwanza ilipokutana na Namungo FC kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa Mkoani Lindi, ilichapwa bao 1-0.