Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Toronto Raptors yaichapa Lakers, LeBron ang'ara NBA

Muktasari:

Kichapo cha Lakers kutoka kwa Toronto Raptors ni cha kwanza baada ya ushindi mechi saba mfululizo za NBA

Dodoma. Mabingwa watetezi wa ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Toronto Raptors ikicheza bila nyota wake wawili Kyle Lowry na Serge Ibaka leo asubuhi wameibuka na ushindi wa pointi 113-104 dhidi ya Los Angeles Lakers uliochezwa uwanja wa Staples Center

Licha ya Raptors kuwakosa Lowry, Ibaka waliokuwa majeruhi, lakini nyota wake wengine Pascal Siakam aliyefunga pointi 24 na ribaundi 11 pamoja na Fred VanVleet aliyefunga pointi 23 na asisti 10 na kuipa ushindi wa 10 mfululizo dhidi ya Lakers.

Lakers iliyopewa nafasi kubwa ya kuendeleza rekodi yake ya kushinda mchezo wa nane mfululizo, ilishindwa kuvunja rekodi ya kufungwa mechi tisa zilizopita dhidi ya Raptors licha ya LeBron James kufunga triple-double ya nne katika mechi tano zilizopita.

LeBron alitoa asisti 15, pointi na ribaundi 13 akifikisha jumla ya triple-double 85 katika nafasi ya tano kihistoria kwa wachezaji wenye idadi nyingi zaidi kwenye ligi hiyo.

Oscar Robertson anaongoza akiwa na triple-double 181 akifuatiwa na Russell Westbrook (139), Magic Johnson (138), Jason Kidd (107) na LeBron James mwenye 85.