Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TOC kuwapiga 'msasa' waandishi wa michezo nchini

Muktasari:

  • Miongoni mwa michezo ambayo iko chini ya TOC ni pamoja na ngumi, kuogelea, mpira wa meza, riadha, kunyanyua vitu vizito na judo.

Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imeandaa semina kwa wanahabari za michezo nchini kwa lengo la kuwaelimisha zaidi kuhusu wajibu wa Kamati hiyo katika sekta ya michezo nchini.

TOC ambayo imekuwa ikiratibu michezo kama ya Olimpiki na Jumuiya ya Madola imekwenda mbali zaidi na kueleza kwamba, baadhi ya wanahabari na wadau wamekuwa na dhanaKamati hiyo iko kwa ajili ya mchezo wa riadha pekee, jambo ambalo si kweli.

"Tukiwaelimisha Wanahabari basi jamii kubwa itakuwa imeelimika kwenye hili," amesema makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo, Henry Tandau.

 Amesema wamekuwa wakiulizwa maswali na baadhi ya wanahabari tofauti tofauti kuhusu majukumu ya TOC, mapato na matumizi na masuala mbalimbali yanayohusu kamati hiyo, jambo ambalo wameona walizungumze kwa upana, kuliko kumjibu mwandishi mmoja mmoja.

"Kuliko kumjibu mmoja mmoja, tumeona ni vema kuandaa semina maalumu kwa wanahabari ambao ni wadau wetu ili wengi wapate elimu kuhusu TOC, semina hii itafanyika mapema wiki ijayo," amrsema Tadau na kuongeza.

"Wapo baadhi yao wanafikiri TOC kazi yake ni kusimamia riadha pekee, jambo ambalo si kweli kuna michezo zaidi ya 16 ambayo iko chini ya ya Kamati hii.

'Hivyo tunamini semina tunayokwenda kuifanya itakuwa na na matokeo chanya na wengi wao kuifahamu vema TOC na wajibu wake  kwenye michezo hiyo ni nini na kazi ya Kamati kwa kuwa maswali tunayoulizwa inaashilia wanahabari wengi hawaifahamu vema TOC," alisema.

Kuhusu mapato na matumizi ya Kamati hiyo, Tandau alisema yamekuwa yakiwekwa wazi kwenye mkutano mkuu wa wanachama ambao hufanyika kwa mujibu wa katiba na ripoti yake inawasilishwa mahala husika.

"TOC ilikuwepo muda mrefu, lakini tulipoingia madarakani, tulianza na ripoti ya kuanzia mwaka 2002 ya mapato na matumizi ambayo yamekaguliwa, ipo na imejitosheleza kwa anayehitaji anapatiwa na kila mkutano mkuu, wanachama wanapewa ripoti hiyo kwa kipidi huska," amesema Tandau.

Hivi karibuni baadhi ya wadau kwenye mitandao ya kijamii walihoji kuhusu mapato na matumizi ya TOC, jambo ambalo Tandau alisema wao kama Taasisi hawatoa taarifa za kiofisi kwenye mitandao ya kijamii ambayo si rasmi kwao.

"Anayehitaji kutaka kufahamu aende ofisini, tapewa majibu stahiki, lakini hatufanyi kazi kwenye mitandao ya kijamii, TOC inafanya kazi kwa weledi na kufuata taratibu na si vinginevyo, tunakaguliwa kwa mujibu wa taratibu," amesema.