Tisa kusepa Yanga Princess
MSIMU ujao huenda Yanga Princess ikakosa huduma ya wachezaji wake tisa walioitumikia misimu kadhaa nyuma.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza ripoti ya kocha wa kikosi hicho, Edina Lema ‘Mourinho’ inahitaji mastaa wapya na kukata tisa.
Mwanaspoti limepata majina ambao tayari wamepewa mkono wa kwaheri na wengine bado wanajadiliwa katika kamati ya utendaji ili kuwaondoa Jangwani.
Wachezaji hao ni Makwidi Fallone, Anastazia Nyandago, Olga Tshilombo, Fatuma Makusanya ‘Cynthia’, Tausi Abdallah, Asphaty Kasindo, Neema Charles, Philomena Daniel na Fatuma Mwisendi ‘Didier.’ Licha ya kuachana nao, hadi sasa Yanga haijasajili mchezaji mpya hata mmoja, lakini ipo kwenye mazungumzo na mastaa wapya kibao akiwemo nahodha wa Serengeti Girls iliyofuzu kucheza Kombe la Dunia, Noella Luhala.