TFF yaula La Liga

Muktasari:
- Taasisi zote mbili zitakuwa na mikutano na semina kubadilishana uelewa wa mchezo ikijumuisha masoko, uongozi wa fedha, utawala na mpango wa mashindano.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira Hispania (RFEF), wamesaini mkataba wa miaka mitatu katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.
Akizungunza na Mwanaspoti, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Clifford Ndimbo alisema lengo kuu la kuingia mkataba huo ni kuhakikisha wanakuwa bega kwa bega katika kuendeleza soka la nchini.
"Katika mchakato huu licha ya kusimamia soka watahakikisha tunakuwa na ligi ya kujitegemea nchini," alisema.
Sanjari na hilo taasisi zote mbili zitakuwa na mikutano na semina kubadilishana uelewa wa mchezo ikijumuisha masoko, uongozi wa fedha, utawala na mpango wa mashindano.
Hafla ya utiaji saini ilifanyika Juni 18, makao makuu ya La Liga mjini, Hispania ilihudhuriwa na Rais wa RFEF, Javier Tebas, Mkurugenzi wa Maendeleo Kimataifa wa RFEF Oscar Mayo, Mwakilishi wa La Liga Tanzania Sami Hanane, Rais wa TFF, Wallace Karia na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura.