Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF yamlima Haji Manara onyo kali

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Boniface Wambura alisema kwamba kamati hiyo ilipopitia jambo hilo na kuamua kutoa onyo kalikwa kiongozi huyo ambaye amekwa na makeke pindi timui yake inapokuwa inacheza.

Dar es Salaam. Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania imempa onyo kali Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara kutokana na kuingia uwanjani kabla na baada ya mechi yao dhidi ya Yanga.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Boniface Wambura alisema kwamba kamati hiyo ilipopitia jambo hilo na kuamua kutoa onyo kalikwa kiongozi huyo ambaye amekwa na makeke pindi timui yake inapokuwa inacheza.

Yanga ilikumbana na kipigo cha bao 1-0 kutoka Simba Jumapili ya wiki iliyopita na kufikisha idadi ya mapambano sita ya watani wa jadi bila kuonja ladha ya ushindi.

Yanga ilipata ushindi wake wa mwisho dhidi ya Simba, Machi 2016, wakati huo kocha wao akiwa Mdachi, Hans Van Pluijm. Tangu hapo ikijitahidi sana ni sare, lakini vipigo imekuwa kawaida kwao.

Bao pekee la kiraka, Erasto Nyoni lilikuwa mwiba tosha kwa Yanga iliyompa ajira kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera ambaye hata hivyo hakukaa benchi kutokana na vibali vyake vya kazi nchini kutokamilika.

Simba sasa imetengeneza wigo wa pointi 14 dhidi ya Yanga na inahitaji ushindi wa mechi mbili tu ili kutangaza ubingwa.