Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF: Manara yuko huru, keshalipa Sh 10 Milioni

Muktasari:

  • Manara leo, ametangaza kurejea kazini baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya TFF.

Saa chache baada ya Msemaji wa Yanga, Haji Manara kutangaza kurejea katika majukumu aliyokuwa anafanya awali, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetoa baraka zote.

Manara leo, ametangaza kurejea kazini baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa kwa miaka miwili iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya TFF.

TFF kupitia Ofisa Habari, Clifford Ndimbo, amesema Manara yuko huru kuendelea na majukumu yake baada ya kukamilika kwa adhabu.

Ndimbo amesema, mbali na Manara kumaliza adhabu, pia amelipa kiasi cha Sh 10 Milioni ikiwa ni faini iliyoambatana na kifungo hicho.

"Manara yuko huru kweli, na hata huo mkutano alioufanya hajakosea kitu kwa kuwa hajafanya kosa lolote kikanuni, adhabu yake ulimalizika," amesema Ndimbo na kuongeza;

"Ukiacha kumalizika kwa adhabu yake pia TFF Ilishapokea malipo ya faini yake ya sh 10 Milioni, malipo hayo aliyafanya wikiendi iliyopita."

Manara alikumbana na adhabu hiyo kutokana kudaiwa kufanya makosa ya kimaadili alipokwaruzana na Rais wa TFF, Wallace Karia, katika Fainali ya Kombe la FA kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga, uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.