Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tarimba awapa neno Yanga

JUZI Jumatatu, Yanga ilitwaa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) matokeo ambayo yamewafurahisha wadhamini wao wakuu Sportpesa ambao wamesema timu hiyo imetimiza malengo yao na wanadeni kubwa msimu ujao.

Yanga iliifunga Azam FC bao 1-0 likifungwa na Kennedy Musonda kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa hivyo timu hiyo ikimaliza msimu kwa kutetea mataji yake yote matatu huku ikifika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba alisema Yanga wana deni kubwa msimu ujao kuhakikisha wanalinda na kuyatetea mafanikio yao ya msinu huu.

"Sisi kama SportPesa tumefurahishwa sana na mafanikio ya Yanga msimu huu, ndani na nje wamefanya vizuri, wamenitimiza malengo yao na yetu, kazi kubwa iliyobaki kwao ni namna ya kuyalinda mafanikio hayo msimu ujao.

"Unapofanya vizuri basi yule anayefanya vibaya anaangalia wapi amejikwaa ili msimu ujao atoe upinzani, hivyo kwa Yanga ni kujiimarisha zaidi kuhakikisha wanajiimarisha kuliko hapa, nafahamu wana mipango mizuri ya msimu ujao hivyo watafanya vyema pia.

"Kama Sportpesa tunawaahidi Yanga kuwapa sapoti kubwa na zile bonasi zao zipo pale pale na tutawapa," alisema Tarimba