Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanimu mbioni kurejea Singida

Muktasari:

  • Tanimu ambaye anacheza beki wa kati na kulia, aliwahi kuwa mmoja wa mastaa waliovutia zaidi katika Ligi Kuu wakati akiitumikia Ihefu ambayo kwa sasa inaitwa Singida Black Stars.

BAADA ya safari yake ya kutafuta mafanikio Ulaya kutokwenda vizuri, beki wa kimataifa wa Nigeria, Benjamin Tanimu yupo mbioni kurudi Singida Black Stars kuanza ukurasa mpya wa maisha ya soka.

Tanimu ambaye anacheza beki wa kati na kulia, aliwahi kuwa mmoja wa mastaa waliovutia zaidi katika Ligi Kuu wakati akiitumikia Ihefu ambayo kwa sasa inaitwa Singida Black Stars.

Katika kipindi hicho alijijengea jina kutokana na uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, uimara katika ukabaji na utulivu wa kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma, kiwango kilichomfanya kuwa mmoja wa mabeki waliotajwa sana na kuvutia macho ya klabu za nje.

Msimu juzi, Singida ilimuuza kwenda England kwa matumaini ya kuendelea kupiga hatua katika soka la kimataifa, lakini safari hiyo haikwenda kama ilivyopangwa baada ya kushindwa kupata nafasi ya ku-cheza.

Na sasa, taarifa za ndani zimeliambia Mwanaspoti kuwa mlango wa kurejea Singida umefunguliwa, hu-ku viongozi wa klabu hiyo wakiamini uzoefu alioupata katika mazingira ya Ulaya unaweza kuwa silaha mpya kwao msimu ujao.

“Singida imeifuata beki huyo ikihitaji huduma yake msimu ujao, hivyo maamuzi yapo kwa mchezaji mwenyewe kwani uongozi umeridhia ujio wake,” kilisema chanzo.

Kwa Singida, kurejea kwa Tanimu kunaonekana kama usajili mpya wenye thamani kubwa kutokana na ukweli kwamba mchezaji huyo tayari anayafahamu mazingira ya soka la Tanzania na matarajio ya mashabiki wa timu hiyo.

Tanimu aliwahi kuwa sehemu muhimu ya safu ya ulinzi ya Ihefu iliyokuwa ikijitahidi kujijenga katika ushindani wa Ligi Kuu na uimara wake uliisaidia timu kujijengea heshima mbele ya vigogo wa soka la Tanzania.

Beki huyo anaweza kupata nafasi katika kikosi cha msimu ujao ikiwa taarifa za kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wa kigeni katika nafasi mbalimbali zitakamilika mwishoni mwa msimu. Miongoni mwa wanaotajwa kuondoka ni Morice Chukwu, Elvis Rupia, Marouf Tchakei na Emmanuel Keyekeh.