Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars kanyaga twende!

Muktasari:

  • Stars inayonolewa na Kocha Mbelgiji, Adel Amrouche inahitaji ushindi kwa aina yoyote ili kuweka matumaini katika kundi hilo kabla ya kurudiana tena jijini Dar es Salaam, Machi 28 ambapo tiketi za pambano hilo zikianza kuuzwa jana Alhamisi na Rais wa Samia Saluhu alinunua 2000
no

HAKUNA namna ni ushindi tu. Mashabiki wa soka wanahesabu saa tu kwa sasa kabla ya kuishuhudia Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ikishuka Uwanja wa Suez Canal, mjini Ismailia, Misri kuvaana na Uganda ‘The Cranes’, huku ikiwa na kiu ya kuona timu hiyo ikipata ushindi ugenini.

Stars na Uganda zinavaana kwenye Kundi F, kuwania Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 zitakazofanyika mwakani nchini Ivory Coast.

Stars inayonolewa na Kocha Mbelgiji, Adel Amrouche inahitaji ushindi kwa aina yoyote ili kuweka matumaini katika kundi hilo kabla ya kurudiana tena jijini Dar es Salaam, Machi 28 ambapo tiketi za pambano hilo zikianza kuuzwa jana Alhamisi na Rais wa Samia Saluhu alinunua 2000.

Katika kundi hilo, Stars iko nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Niger mchezo uliochezwa nchini Niger, ikipoteza kwa mabao 2-0 mbele ya vinara wa kundi hilo, Algeria kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

‘The Cranes’ ina pointi moja pia baada ya kucheza michezo miwili na kati ya hiyo imetoka sare mmoja na kupoteza mmoja huku Algeria ikiwa kinara na pointi sita wakati Niger ina pointi mbili.


MZUKA WA SH 500 MILIONI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana alisema serikali itatoa Sh 500 milioni kwa timu hiyo endapo itafuzu ikiwa ni sehemu ya motisha kama ilivyofanya mara ya mwisho mwaka 2019.

Huu ni mwendelezo wa Serikali chini ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa motisha baada ya kununua kila bao Sh 5milioni kwenye michuano ya kimataifa kwa timu za Simba na Yanga.

Kiu ya mashabiki ni kuona kikosi hicho kinakuwa na mwendelezo mzuri baada ya kufanya hivyo kule nchini Misri chini ya aliyekuwa Kocha Mkuu Mnigeria, Emmanuel Amunike kufuatia kupita miaka 39.


REKODI CHANGAMOTO

Stars inaingia katika mchezo huu ikiwa haina rekodi nzuri pindi inapocheza na ‘The Cranes’ kwani kwenye michezo 19 zilipokutana Uganda imeshinda 12, sare minne na kupoteza mitatu tu.

Rekodi zinaonyesha pia Uganda imefanya vizuri inapocheza uwanja wake wa nyumbani kwa sababu katika michezo 10 imeshinda sita, sare mitatu huku Stars ikiambulia ushindi mara moja.

Kwenye uwanja wa ugenini timu hizo zimekutana mara tisa ambapo kati ya hiyo pia Stars imekuwa na wakati mgumu kwani imeshinda michezo miwili tu, sare moja na kuchezea kichapo mara sita.


MWAMUZI WA AFCON

Mwamuzi, Ahmad Imtehaz Heeralall wa Mauritius ndiye aliyepangiwa kuchezesha mchezo huo huku akikumbukwa zaidi kwani alishawahi kuchezesha Stars dhidi ya Kenya mwaka 2019 kule Misri. Katika mchezo huo wa AFCON uliopigwa Juni 29, Stars ilipoteza kwa mabao 3-2 ikiwa kwenye Kundi ‘C’ la michuano hiyo sambamba na timu za Algeria iliyomaliza kinara na kufuatiwa na Senegal.


MZUKA MWINGI

Mastaa wa timu hiyo wakiongozwa na nahodha, Mbwana Samatta wamekuwa na mzuka mwingi kwa ajili ya pambano hilo litakalopigwa kuanzia saa 11:00 jioni, lakini kubwa kutaka kulipa kisasi dhidi ya Uganda walioizuia Tanzania kwenda kwenye fainali za CHAN 2022. Uganda iliifunga Tanzania mabao 3-0 katika mechi ya kwanza ya mchujo ya mbio za kwenda Algeria kisha kuinyoa tena bao 1-0 na kuing’oa kwa jumla ya mabao 4-0, hivyo mechi ya leo ni kisasi kwa nyota wa Stars wanaojua kupoteza ugenini itazidi kuiweka pabaya timu hiyo katika kundi hilo.

Katika kundi hilo, Algeria ndio inayoongoza msimamo ikiwa na pointi sita ambayo usiku wa kuamkia leo ilikuwa nyumbani kuvaana na Niger inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi mbili, hivyo kusaidia kuitia mzuka Stars kupambana kujiweka pazuri kwenye msimamo wa kundi hilo.


MSIKIE AMROUCHE

Kocha wa Taifa Stars, Adel Amrouche alisema licha ya maandalizi ya muda mchache ila amefurahia uwajibikaji wa mchezaji mmoja mmoja huku akiamini mastaa wake wana uwezo wa kuibuka na ushindi.

“Tumekuwa na maandalizi mazuri yaliyojikita kwenye mbinu juu ya namna ya kucheza vizuri na kupata matokeo chanya kwani nitafurahi tukishinda michezo yote pia miwili dhidi yao,” alisema.