Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Musonda kuna kitu

MUSONDA Pict

Muktasari:

  • Hata hivyo, ubingwa utanogeshwa zaidi na utamu Msimbazi kwani mashabiki wa Wekundu hao watakuwa wamebakiza pia mechi tatu nne za Ligi Kuu Bara, huku wakiwa tayari wameshakula viporo vyao vinne bila shida.

MAMBO ni moto na muda ni mchache. Simba itakuwa Morocco kukipiga na RS Berkane katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu na yenye hisia tofauti ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwani wiki ijayo itakuwa jijini Dar es Salaam kukamilisha ratiba na kukabidhiwa ndoo ya ubingwa.

Hata hivyo, ubingwa utanogeshwa zaidi na utamu Msimbazi kwani mashabiki wa Wekundu hao watakuwa wamebakiza pia mechi tatu nne za Ligi Kuu Bara, huku wakiwa tayari wameshakula viporo vyao vinne bila shida.

Lakini, taarifa ikufikie kwamba Simba imerudi tena kwa mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda ikiamini kwamba bado Mzambia huyo hajatumika sawasawa Jangwani.

Musonda ambaye huu ni msimu wake wa tatu ndani ya Yanga, ni miongoni mwa mastaa ambao wako mbioni kumaliza mikataba mwishoni mwa msimu huu.

Hii sio mara ya kwanza kwa Wekundu wa Msimbazi kutaka saini ya mshambuliaji huyo, kwani hata msimu uliopita walihitaji kumchukua, lakini mkataba wake na Yanga ulikuwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja ambao ndio unaomalizika.


ISHU YA NAMBA

Katika nafasi anayoichezea Musonda yupo na mastaa wengine wawili ambao ni Clement Mzize ambaye kabla ya mechi ya jana alikuwa ametupia mabao 13 na Prince Dube (12), ambao ndio wanacheza muda mwingi.

Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kufanya mahojiano na gazeti hili alisema namba yake pendwa uwanjani ni tisa, japokuwa kocha hamtumii sana katika eneo hilo.

"Kocha ananichezesha kama winga au nyuma ya mshambuliaji wa mwisho, jambo ambalo halinipi uhuru wa kucheza ninavyotaka. Mimi ni mshambuliaji niko huru zaidi kucheza namba tisa, kwani hapo ndio najiona kuwa naweza nikafanya kitu kikubwa tofauti na hizi nafasi zingine," alikaririwa wakati huo akisema Yanga ikiwa chini ya kocha Saed Ramovic.


SABABU ZA SIMBA KURUDI

Taarifa za ndani zinasema Simba bado inaamini Musonda ana vitu ambavyo bado havijatumika anapoichezea Yanga, japo ina washambuliaji.

"Simba inataka mshambuliaji wa mwisho atakayekuja kufanya vizuri na kati ya hao kuna Musonda ambaye hana historia ya majeraha ya muda mrefu, lakini pia kama akitumika mshambuliaji namba tisa atafanya vizuri," kimesema chanzo kutoka Simba.


NAFASI YAKE SIMBA

Katika msimu huu Simba ina mastaa wawili wa kigeni ambao wanacheza eneo la ushambuliaji akiwemo Leonel Ateba na Steven Mukwala.

Rekodi za washambuliaji wa Simba sio za kinyonge huku Mukwala akiwa na mabao 11 na Ateba akiwa nayo 12.

Kwa upande wa Musonda anayo matatu, hivyo mastaa wanaocheza katika eneo hilo pia wamempiku Mzambia huyo kama ilivyo Yanga.


SIMBA INAUHITAJI WA MUSONDA?

Licha wa washambuliaji wa Simba kuwa na rekodi nzuri ya mabao, lakini bado inashida ya umaliziaji jambo ambalo limekuwa likiwaweka kwenye wakati mgumu Ateba na Mukwala.

Lakini, mipango ya Simba ni kupunguza baadhi ya wachezaji ifikapo dirisha la usajili wa majira ya kiangazi akiwemo Agustine Okejepha ambaye katika eneo lake kuna mastaa kama Fabrice Ngoma na Yusuf Kagoma walioonyesha uwezo mkubwa na kupatana wakiwa uwanjani.

Inadaiwa kuwa hesabu za mabosi wa Yanga kwa Musonda ni kumpeleka Singida Black Star ambako watamchukua mshambuliaji mpya wa kikosi hicho, Jonathan Souwah.


REKODI ZAKE

Musonda tangu atue Yanga amefunga mabao mawili msimu wa kwanza, matano ule wa pili tofauti na alipotoka Power Dynamos alikotoka akiwa nayo 10 katika msimu wa 2022/23.


KENNEDY MUSONDA

Mechi: 13

Dakika: 359

Asisti: 00

Mabao: 03