Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tabora United yaziwinda pointi za Simba

MACHO, hesabu na mipango yote ya Tabora United kwa sasa ni dhidi ya Simba katika mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara huku lengo kubwa likiwa ni kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu mbele ya mnyama.

Timu hizo zitakutana Desemba 29, mwaka huu katika Uwanja wa Alli Hassan Mwinyi, mkoani Tabora baada ya mapumziko ya takribani miezi miwili kupisha kalenda ya mechi za kimataifa za timu za taifa na Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza Novemba 25, mwaka huu.

Tabora United imekuwa na matokeo mazuri msimu huu ikiwa haijapoteza mchezo wowote nyumbani ikishinda miwili na sare moja na inakamata nafasi ya nane na alama 11 baada ya michezo tisa.

Akizungumza juzi baada ya sare na Geita Gold, Kocha msaidizi wa Tabora United, Henry Mkanwa, alisema benchi la ufundi halilali wala kupumzika bali linayatumia mapumziko hayo kufanya marekebisho katika mapungufu waliyoyaona kwenye mchezo huo kabla ya kuivaa Simba ili wasiingie kinyonge.

“Sisi hatupumziki tunarudi kuendelea na kazi kufanya mabadiliko katika makosa ambayo nimeyaona leo, nina imani nitayafanyia kazi yote ili mechi na Simba nisiwe na makosa. Mashabiki naomba waisapoti timu yao wawape nguvu zaidi vijana wao katika mechi zetu nyumbani,”

“kwa kweli wachezaji wangu wamebadilika sana tumefaulu leo kupata pointi moja siyo kitu kidogo uwanja wa ugenini kwahiyo tumefaulu na wachezaji wangu wamefuata maelekezo wamecheza vizuri na tumepata pointi moja kwenye timu yetu kila mchezaji lazima acheze na kila mmoja anataka kuisaidia timu,” alisema Mkanwa

Nahodha wa timu hiyo, Said Mbatty, alisema “Mechi zote ugenini zilikuwa ngumu tunashukuru kwa kile tulichokipata, tumejipanga vizuri naamini mechi za nyumbani tutapata matokeo mazuri, mashabiki wetu wasichoke hii ni timu yao.”