Sven: Morrison anawatosha

Tuesday September 29 2020
sven pic

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema anavutiwa na burudani ya Bernard Morrison pindi wanapokuwa uwanjani.

Sven alisema si jambo baya endapo Morrison atakuwa akionyesha madaha ambayo yana faida kwa timu haswa pale tunaposhambulia kwani muda mwingine ndio hutengeneza nafasi za mabao.

“Morrison ni mchezaji mzuri mwenye kipaji tangu amefika hapa amekuwa akilionyesha hilo katika mazoezi na mechi, nina imani siku zijazo atakuja kufanya mambo bora zaidi,” alisema.

“Morrison hakuwa na maandalizi mazuri ya msimu kama ambavyo walifanya wachezaji wengine ndani ya kikosi. Kwake yalikuwa mafupi mno. Kwenye timu nahitaji zaidi umoja ambao Morrison ameonyesha. Katika mechi na Gwambina alipata nafasi ya kufunga akiwa amebaki na kipa akaamua kutoa pasi ya mwisho kwa mwenzake, jambo ambalo kama wachezaji wote wakiwa na hali kama hiyo tunakwenda kutwaa tena ubingwa msimu huu.

“Ukim

uangalia Morrison hachezi kiuwezo wake binafsi bali anacheza kwa kushirikiana na wenzake kitimu zaidi,” alisema Sven na kuongeza kuwa Morrison ameongeza ushindani haswa katika eneo la ushambuliaji kwa kufanya kila ambaye anacheza katika nafasi hiyo akipata nafasi kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Advertisement

“Katika kikosi Morrison nategemea kumuona akifanya mambo mengi mazuri na akionyesha kiwango bora zaidi ya wakati huu, tunakwenda kucheza ugenini nategemea kuona timu yangu ikicheza katika kiwango ambacho tulikionyesha dhidi Biashara United na Gwambina, ingawa natambua hatutacheza mechi ambayo inafanana,” aliongezea.

 

Advertisement