Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sure boy aagwa rasmi Azam

AZAM FC, wametangaza rasmi kuachana na nahodha wao msaidizi, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ baada ya kudumu katika kikosi hicho kwa muda wa miaka 14.

Wiki kadhaa zilizopita Uongozi wa Azam ulimsimamisha Sure Boy na wachezaji wengine Mudathir Yahya na Aggrey Morris kwa masuala ya kinidhamu.

Baada ya muda fulani kupita wachezaji hao walitakiwa kurudi kujiunga na wenzao baada ya kusamehewa Morris na Mudathir walirudi lakini Sure Boy alikataa.

Baada ya kukataa kurudi Sure Boy aliomba kuondoka katika klabu hiyo na alifuata taratibu zote kama ambavyo ilitakuwa ili kwenda katika maisha yake mapya.

Inaelezwa Sure Boy ameshakubaliana kila kitu na Yanga kinacho subiriwa ni utaratibu kukamilika kisha kumtangaza nyota hiyo.

Kupitia ukurasa rasmi wa Azam walindika,

Uongozi wa klabu ya Azam FC umesema mchezaji Salum Abubakary 'Sure boy' , alasiri ya leo Desemba 22,  Azam amechukua barua yake ya kuruhusiwa kuondoka katika timu hiyo.

Sure boy amekabidhiwa barua hiyo na afisa mtendaji mkuu, Abdulkarim Amin Popat.

"Kwa barua hiyo, ni rasmi sasa kwamba Salum Abubakary siyo tena mchezaji wa Azam Football Club.," wamesema Azam