Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars yatoka mikono mitupu Chalenji

Muktasari:

Katika hatua ya makundi, Kilimanjaro Stars iliruhusu bao moja tu ambalo walifungwa dhidi ya Kenya na wakafungwa lingine katika hatua ya nusu fainali dhidi ya Uganda.

Mabao mawili ya Kenneth Muguna na Abdallah Hassan  yameifanya timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kutoka mikono mitupu katika mashindano ya Chalenji baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kenya katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu.
Katika mchezo huo ulioanza saa 7:00 mchana, Kenya walitumia walitumia vyema makosa binafsi ya wachezaji wa Stars, kuweza kupachika mabao hayo ambayo yameifanya Kenya imalize kipindi cha kwanza ikiwa  inaongoza kwa mabao 2-0 huku bao la kufutia machozi la Kilimanjaro Stars likifungwa kipindi cha pili na Gadiel Michael.
Ikionekana kama inacheza kukamilisha ratiba, Kilimanjaro Stars imeonekana kushindwa kuchangamka na kundi kubwa la wachezaji wake linaonekana  kucheza ili mradi tu, hali ambayo imetumiwa vyema na Kenya kuwaadhibu.
Kenya ambao walionekana kucheza kwa hesabu zaidi, walikuwa wepesi katika kuanzisha mpira kila wanapoupokonya kutoka kwa wachezaji wa Kilimanjaro Stars na kushambulia kwa haraka jambo ambalo limeonekana kuzaa matunda kwa upande wao.
Dakika ya 16 tu ya mchezo, Muguna aliwainua vitini Kenya baada ya kuwapachikia bao la kuongoza akiunganisha kwa shuti la wastani, pasi ya Oscar Wamalwa.
Kabla ya kupiga pasi hiyo, Wamalwa alimzidi ujanja Kelvin Yondani ambaye alishindwa kumkaba na kumpiga chenga kisha kuupeleka mpira huo kwa Muguna ambaye hakufanya ajizi kuujaza wavuni.
Dakika 12 baadaye, Kenya nusura waandike bao la pili lakini kiungo wake Lawrence Juma akiwa analitazama lango baada ya kupokea pasi ya Moses Mudavadi, alipiga shuti lililotoka nje.
Stars haikuonekana kujifunza kutokana na bao la kwanza na badala yake ikaendelea kurudia makosa yaleyale ya kupiga pasi ambazo hazikufikia walengwa lakini pia kupoteza mipira mara kwa mara.
Uzembe wa kiungo Mzamiru Yassin kuchelewa kuachia mpira kwa haraka pindi Kilimanjaro Stars ilipokuwa inaumiliki, uliigharimu timu kwa kuwa chanzo cha Kenya kufunga bao la pili.
Wakati idadi kubwa ya wachezaji ikiwa imeuvuka mstari unaogawa uwanja na kuwa kwenye nusu ya Kenya, Mzamiru ambaye alichelewa kutoa pasi, alijikuta akiporwa mpira na Antony Wambani ambaye alimpasia kwa haraka Hassan aliyeimalizia kiustadi kwa staili ya kubetua na kuujaza wavuni.
Baada ya kuingia bao hilo, Stars ilijaribu kujitutumua na kulazimisha kupenya safu ya ulinzi ya Kenya lakini ilikosa ubunifu na kupelekea ipoteze mipira mingi ya mwisho jirani na lango la Kenya.