Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars waonja fitina za Waarabu

Kipa wa Taifa Stars Shabaani Kado ambaye usiku wa kuamkia leo Jumamosi alikuwa nyota wa mchezo dhidi ya Algeria kwani licha ya matokeo ya 1-1 alifanya kazi kubwa kuokoa michomo mbalimbali ya wapinzani.

Samson Mfalila, Algiers TAIFA Stars ambayo jana usiku ilikuwa ikichuana na wenyeji wao, Algeria ilijikuta ikikabiliana na fitina za Waalgeria baada ya basi lao kutelekezwa na dereva wake kutoweka akiacha mlango wazi na kuwaruhusu mashabiki wa hapa kurandaranda pembeni mwa basi hilo. Viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walioko hapa walikutana na kituko hicho na kuwajia juu wenyeji wao walionywea na kulazimika kulibadili basi hilo. Kikosi cha Stars kilitakiwa kuondoka kwa basi hilo kwenda kwenye mazoezi ya usiku yaliyokuwa yakifanyika kwenye Uwanja wa Mustapha Tchaker ulioko katika mji wa Blida ili kujiandaa na mechi ya jana, dhidi ya Algeria. Mwandishi wa Mwananchi aliyeko hapa alishuhudia tukio hilo juzi, Alhamisi saa10 jioni za hapa (saa 12 jioni kwa saa za Tanzania) ambapo dereva basi hilo aliamua kulitekeleza basi hilo na kutoweka. Kilichotia hofu zaidi ni mashabiki wa soka wa hapa wapatao 12 waliokuwa wamezunguka basi hilo lililoandaliwa maalum kuwabeba wachezaji bila ya kujulikana walikuwa na dhamira gani. Basi hilo lilikuwa limegeeshwa nje ya hoteli ya Hilton Alger ambako msafara wa Stars ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo ulikuwa umefikia hapo. Kitendo hicho kilimkasirisha Kiondo, aliyekuwa amefuatana na ofisa wa Habari wa TFF, Florian Kaijage na Issa Matimbwa, ambaye ni Mtanzania anayeishi Algeria. Wao pia walishtushwa na fitina za timu za Afrika Kaskazini ambazo wamekuwa wakizifanyia timu za Tanzania. Kaijage na Matimbwa walimvaa ofisa wa Shirikisho la Soka la Algeria aliyekuwa na jukumu la kuangalia masuala mbalimbali ya Stars, aliyejulikana kwa jina la Salah, ambaye mara ya kwanza alionyesha kudharau malalamiko ya maofisa wa Tanzania. Mashabiki baada ya kuona kuwa Watanzania wamewafuma, wakatawanyika mmoja mmoja, ingawa haikujikana wazi walitaka kufanya nini. Salah alitoa maneno makali, ambapo suala hilo lilifikia hadi walinzi wa hoteli ya Hilton kuingilia kati ili kumaliza tatizo hilo. Walinzi hao waliwahakikishia Stars kuwa mashabiki hao wa waliokuwa wamezunguka basi lao wasingefanya chochote kwenye basi hili, bali walikuwa wamekaa tu na hawakuwa wamefanya kitu chochote kibaya. Walipoulizwa kwanini dereva alikuwa amelitekeleza basi hilo huku mlango ukiwa mbovu, walijitetea kwa sababu ambazo hazieleweki. Waliongeza zaidi katika maelezo yao kuwa eneo hilo lilikuwa linalindwa na kamera za usalama (CCTV) ndio maana haikuwa rahisi kwa yoyote kufanya kitu chochote kibaya kwenye basi hilo. Salah, akaahidi kuwa basi hilo lingebadilishwa kutokana na ukweli kuwa maofisa wa Stars walishikilia kutumia basi lenye mlango mbovu. Basi hilo lilipokuwa likibadilishwa , Salah akaibuka na maneno ya kejeli;"Haya tumewabadilishia basi msije mkafungwa mkasingizia kuwa mlipewa basi bovu na mashabiki walilifanyia fujo." Kwa upande wao, wachezaji wa Stars chini ya Jan Poulsen wamekuwa wakijinoa kwa mazoezi ya usiku. Msafara wa timu hiyo ulipotua mchana Jumatano iliyopita ulianza kwa mazoezi ya kutembea jioni katika hoteli ya Hilton Alger ilipofikia timu hiyo. Poulsen aliwapumzisha wachezaji wake na baadaye siku hiyo na kuwapeleka saa nne usiku kwenye uwanja wa Roiba ulioko kama kilomita 15 nje ya jiji la Algeria kwa ajili ya mazoezi ya usiku. Kikosi cha Stars hakikukifanya mazoezi Alhamisi asubuhi, usiku wake siku hiyo kilipelekwa saa nne kwenye uwanja wa Mustapha Tchaker ulioko kama kilomita 45 kutoka jijini Algiers, mahali ambako wenyeji wanapaita machinjioni. Matukio ya fitina za Waarabu ni kama yale ya mwaka 1974, ambako Simba ilitolewa na Mehalla el-Kubra ya Misri, kipa wake Athumani Mambosasa alifanyiwa vurugu. Pia, Yanga ilikumbana na dhoruba za aina hiyo mwaka 1992 kwenye mechi ya Klabu Bingwa Afrika jijini Cairo, Misri dhidi ya Al-Ahly ambapo kipa wake alivuliwa glovu na Yanga kuchapwa mabao 5-0, yote yakiwa yamefungwa kipindi cha pili.