Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stars, The Cranes patachimbika

Muktasari:

  • Stars inahitaji ushindi ili kuweka matumaini hai katika kundi F kabla ya kurudiana tena jijini Dar es Salaam Machi 28
no

TIMU ya taifa 'Taifa Stars' ina kibarua kizito leo cha kuhakikisha inashinda mchezo dhidi ya Uganda ambao utapigwa nchini Misri kwa ajili ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) itakayofanyika mwakani Ivory Coast.

Stars inahitaji ushindi ili kuweka matumaini hai katika kundi F kabla ya kurudiana tena jijini Dar es Salaam Machi 28.
Mwanaspoti linakuletea uchambuzi muhimu wakati kikosi hicho kikitarajiwa kufanya makubwa ili kuiletea nchi heshima.


KUNDI LA MTEGO
Stars ili iweke matumaini yake hai ya kusonga mbele inahitaji kuhakikisha inashinda mechi zote mbili dhidi ya Uganda huku kwa wakati huo iiombee njaa Niger kufungwa na Algeria kwenye michezo wanayokutana baina yao.
Stars inashika nafasi ya tatu katika kundi F ikiwa na pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Niger mchezo uliopigwa nchini Niger huku mechi ya pili ikipoteza 2-0 na Algeria kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa upande wa Uganda ina pointi moja pia baada ya kucheza michezo miwili ambapo kati ya hiyo imetoa sare mmoja na kupoteza mmoja wakati Algeria ndio kinara na pointi sita ikifuatiwa na Niger yenye pointi mbili.


BENCHI JIPYA LA UFUNDI
Stars inaingia katika mchezo huu ikiwa na benchi jipya la ufundi chini ya Kocha Mkuu Mbelgiji, Adel Amrouche mwenye asili ya Algeria akibeba matumaini makubwa ya Watanzania kutokana na uzoefu mkubwa wa Soka la Afrika.

Amrouche amewahi kuteuliwa kocha bora wa Afrika Mashariki mwaka 2013 wakati akiinoa na kuipa Kenya 'Harambee Stars' ubingwa wa Cecafa Challenge ingawa kabla ya hapo alifika nusu fainali mara mbili akiifundisha timu ya Burundi.
Tangu kutimuliwa kwa Kim Poulsen Agosti 29, mwaka jana Stars ilikuwa chini ya kocha wa muda Mzambia, Hanour Janza ambaye naye aliamua kurudi kwao baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Klabu ya Zesco United.


KUJIRUDIA YA 2019
Hili ndilo swali ambalo mashabiki wengi wa soka nchini wanajiuliza kwenye kikosi hicho kama kitafuzu kama ilivyofanya mwaka 2019 kule Misri na kuvunja rekodi iliyodumu miaka 39 tangu mara ya mwisho iliposhiriki.

Mafanikio hayo ya Stars yalimfanya Amunike afikie rekodi iliyowekwa na Mpoland, Slawomir Wolk aliyewezesha Tanzania kucheza fainali za mwaka 1980 nchini Nigeria ambapo kabla ya hapo Taifa lilifundishwa na makocha 21.


MCHEZO WA KISASI
Mchezo huu ni wa kisasi kwa Stars kwani kabla ya kukutana kwenye michuano hii ilishindwa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani (CHAN) mwaka jana baada ya kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0.

Kichapo hicho kilisababisha aliyekuwa Kocha Mkuu, Mdenmark, Kim Poulsen kutimuliwa na Mzambia, Hanour Janza kupewa timu.