Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JKT Tanzania yaiweka pabaya Fountain Gate

JKT Pict

Muktasari:

  • Hiyo ni baada ya JKT Tanzania kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo uliofanyika leo Jumanne.

JKT Tanzania imezidi kuiweka pabaya Fountain Gate katika msimamo wa Ligi Kuu Bara huku zikisalia mechi mbili kumaliza msimu huu.

Hiyo ni baada ya JKT Tanzania kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Meja Jenerali Isamuhyo kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo uliofanyika leo  Jumanne.

Kipigo hicho kimeifanya Fountain Gate kusalia na pointi 29 ikiendelea kuwepo kwenye mstari wa kucheza mechi za mtoano kupambania kutoshuka daraja, huku JKT Tanzania ikihitaji pointi moja pekee katika mechi mbili zilizobaki ili kuwa salama zaidi. Kwa sasa ina pointi 35 baada ya mechi 28.

Fountain Gate yenye maskani yake Manyara, mechi mbili za kupambana itoke nafasi iliyopo sasa itacheza dhidi ya Coastal Union (Juni 18) ugenini na Azam (Juni 22) nyumbani ambapo inahitaji kushinda zote, huku ikiziombea mabaya Pamba Jiji, KMC na Tanzania Prisons.

Katika mchezo ambao Fountain ilipoteza, JKT Tanzania ilikuwa na siku nzuri kwani hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mohamed Bakari dakika ya 7 na Shiza Kichuya dakika ya 45. Kipindi cha pili, JKT Tanzania ikaongeza bao la tatu dakika ya 59 mfungaji akiwa Edward Songo.

Mfungaji wa bao pekee la Fountain Gate ni William Edgar dakika ya 87 ambalo limemfanya mshambuliaji huyo kumaliza ukame wa mabao baada ya kutocheka na nyavu kwa takribani siku 146 kwani kabla ya hapo mara ya mwisho alifunga Desemba 13, 2024 wakati Fountain Gate ikishnda 3-2 dhidi ya Coastal Union.

Upekee wa bao hilo lililoondoa ukame kwa Edgar ni namna ambavyo lilipatikana kwani mshambuliaji huyo mara ya mwisho alifunga tarehe 13, kisha akafunga tena tarehe kama hiyo japo mwezi na mwaka tofauti.

Kama haitoshi, mara ya mwisho alifunga katika mchezo ulioanza saa 8:00 mchana, pia amecheka tena na nyavu mechi ikichezwa muda huo.