Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Stand United: Tutawaheshimu Mtibwa Sugar

Muktasari:

  • Mchezo huo uliopangwa kuchezwa kesho, Jumatano, Februari 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani, utawakutanisha Mtibwa Sugar na Stand United ya Shinyanga huku kila moja ikiutumia kujiimarisha kutokana na ligi inayoshiriki.

Uongozi wa timu ya soka ya Stand United ya mjini Shinyanga kupitia kwa meneja wake, Fred Masai umesema wamejipanga kupata matokeo chanya katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) watakapocheza na Mtibwa na wataingia mchezoni kwa kuiheshimu timu hiyo.

Mchezo huo uliopangwa kuchezwa kesho, Jumatano, Februari 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Turiani, utawakutanisha Mtibwa Sugar na Stand United ya Shinyanga huku kila moja ikiutumia kujiimarisha kutokana na ligi inayoshiriki.

Masai amesema: “Tayari tumewasili Morogoro na tumejiandaa kikamilifu kucheza na Mtibwa Sugar na tutaenda kwenye mchezo huo tukiwaheshimu, lakini shahaba yetu ni kucheza robo fainali   msimu huu kama tulivyowahi kucheza na Simba 2020 hatua ya 16 bora ambapo tulishindwa kufika robo fainali kwa kufungwa penalti 3-2 baada ya dakika 90 kuisha tukiwa tumefungana bao 1-1.”

“Tunatambua Mtibwa ni timu kubwa na kongwe na wenyewe wamewahi kucheza fainali na Singida United, lakini tumejipanga  ili kupata matokeo pamoja na wamekuwa hawana historia ya matokeo mazuri kwenye michezo ya ligi wanayocheza.”