Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SportPesa Super Cup mambo yote hadharani

Ofisa Uhusiano wa kampuni ya SportPesa, Sabrina Msuya

Muktasari:

  • Mpango mzima wa mwaka huu, unatarajiwa kuanikwa hadharani leo ambapo SportPesa itazitangaza timu nne za Tanzania Bara zitakazoshiriki, zikiwamo tatu wanazozithamini za Yanga, Simba na Singida United.

ILE michuano iliyobamba kinoma mwaka jana ya SportPesa Super Cup iliyoshuhudia Everton ya England ikitua nchini na kuliamsha dude na mabingwa wa michuano hiyo Gor Mahia, mambo yameiva.

Mpango mzima wa mwaka huu, unatarajiwa kuanikwa hadharani leo ambapo SportPesa itazitangaza timu nne za Tanzania Bara zitakazoshiriki, zikiwamo tatu wanazozithamini za Yanga, Simba na Singida United.

Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Sabrina Msuya alisema kila kitu kitawekwa hadharani leo saa 4 asubuhi kwenye makao makuu ya SportPesa.

“Je unajua timu ya nne itakuwa ipi?

Kila kitu kitawekwa hadharani kesho (leo),” alisisitiza Sabrina baada ya kutaka aitaje timu hiyo ya nne.

Katika michuano ya mwaka jana iliyoshirikisha timu nane, nne za Kenya na nyingine za Tanzania, mbali na Simba, Yanga na Singida timu nyingine ya nne ilikuwa ni Jang’ombe Boys kutoka Zanzibar.

Kenya iliwakilishwa na klabu za Gor Mahia, AFC Leopards zinazothaminiwa na Sportpesa, Tusker FC na Nakuru AllStars.