Jaruph afurahishwa na mwaliko wa Oman

Muktasari:
- Ain inashiriki Ligi Kuu ya Morocco na Mtanzania huyo alijiunga nayo wakati ligi hiyo inaenda mwishoni na ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika mechi 10 alifunga mabao manane na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza ligi hiyo na kufunga hat-trick.
KOCHA wa timu ya taifa ya Soka la Ufukweni ya Tanzania (Beach Soccer), Jaruph Juma amesema kualikwa Oman kutawaongezea kitu kutokana na nchi hiyo kupiga hatua katika mchezo huo.
Tanzania imealikwa nchini humo kama sehemu ya programu ya kubadilishana uzoefu kwa vitendo baina ya nchi hizo.
Akizungumzia ziara hiyo alisema "Ni jambo zuri kujifunza kwa nchi zilizoendelea, soka la ufukweni kwa Tanzania linafanya vizuri kwa hiyo ni jambo zuri kuongeza uzoefu kwa nchi zilizoendelea kama Oman na itakuwa na faida kwangu pia kama kocha."
Ikumbukwe Jaruph mbali ya kuwa kocha ni mchezaji anayekipiga Ain Diab ya Morocco.
Ain inashiriki Ligi Kuu ya Morocco na Mtanzania huyo alijiunga nayo wakati ligi hiyo inaenda mwishoni na ukiwa ni msimu wake wa kwanza katika mechi 10 alifunga mabao manane na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kucheza ligi hiyo na kufunga hat-trick.