Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sita wakalia kuti kavu KMC FC

KMC Pict

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Mkoti Mwakasungura alisema, nyota hao wamemaliza mikataba na watakuwa na majadiliano yatakayotanguliwa na maamuzi ya uongozi na benchi la ufundi.

MASTAA sita wakalia kuti kavu KMC,wasubiri kikao cha mabosi kufanya maamuzi ya hatima ya kusalia kwao ndani ya klabu hiyo, baada ya mikataba yao kumalizika.

Akizungumza na Mwanaspoti Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Mkoti Mwakasungura alisema, nyota hao wamemaliza mikataba na watakuwa na majadiliano yatakayotanguliwa na maamuzi ya uongozi na benchi la ufundi.

Alisema maamuzi hayo juu ya hatima ya wachezaji yatafanyika mapema wiki hii ili waweze kuwapa muda watakaoondoka kusaka timu.

“Mapema wiki hii ni kweli tutakuwa na kikao kama ulivyosema hapo na tutajadili mambo mengi sio tu kuhusu wachezaji ambao mikataba yao imekwisha.

“Tutakuwa na benchi la ufundi ili wao pia watoe maamuzi yao juu ya wachezaji hao kama bado wanawahitaji.”

Miongoni mwa mastaa ambao wamemaliza mikataba yao yuko beki wa zamani Yanga Andrew Vincent ‘Dante’, ambaye tayari ameshapata dili Mbeya City na Mtibwa Sugar.

Kupitia Mwanaspoti iliandika; “Beki huyo mkongwe tayari ameshaanza mazungumzo na mabosi wa Mtibwa ili kufanikisha usajili huo wa kunasa saini yake kwa ajili ya msimu ujao.”

Mastaa waliomaliza mikataba yao ni; Fredrick Tangalo (beki wa kati), Wilbol Maseke (kipa), Shaban Chilunda (mshambuliaji), Austin Ajoh (mshambuliaji raia wa Cameroon), Vincent Abubakar (winga), Andrew Vincent ‘Dante’(beki ambaye tayari ameaga anaondoka) na Rahim Shomari (beki wa kushoto).

KMC ilimaliza ligi nafasi ya 10 katika msimamo,ikiwa imejizolea pointi 35, ikishinda michezo tisa, sare nane na kupoteza 13 katika mechi 30 iliyocheza.