Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Said Jr ataka kuvunja rekodi ya mabao

SAID Pict

Muktasari:

  • Said Jr aliyejiunga na Malaysia FC msimu uliopita, amesema kama mshambuliaji kila msimu anajiwekea malengo ya kuvunja rekodi ya msimu uliopita.

MSHAMBULIAJI wa Malaysia FC, Said Khamis Jr, amesema malengo yake msimu wa 2026-2027 ni kufunga zaidi ya mabao 20 na kuweka rekodi mpya ya ufungaji bora.

Said Jr aliyejiunga na Malaysia FC msimu uliopita, amesema kama mshambuliaji kila msimu anajiwekea malengo ya kuvunja rekodi ya msimu uliopita.

Akizungumza na Mwanaspoti, mshambuliaji huyo amesema anatambua kazi iliyopo mbele yake si rahisi, lakini anaamini malengo yanaweza kutimia kwa juhudi na nidhamu.

"Naamini kwa uwezo wa Mungu itawezekana. Ni ngumu kuvunja rekodi yangu ya msimu uliopita, lakini haiwezekani kusema haiwezekani. Ukiweka na malengo na kufanya kazi kwa bidii unaweza kuyafikia," amesema Said Jr.

Kuhusu maandalizi ya msimu mpya, amesema bado uongozi wa ligi haujatangaza tarehe ya kuanza kwa mashindano, lakini ameendelea kufanya mazoezi binafsi ili kurejea kambini akiwa kwenye kiwango bora.

"Bado haijatangazwa ligi inaanza lini, hivyo naendelea na mazoezi binafsi ili nirudi nikiwa fiti na tayari kuisaidia timu," amesema.

Msimu uliopita Said Jr ambaye aliwahi kuitumikia Mbao FC, alicheza mechi 25 akifunga mabao 21.