Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yawatega makipa watatu


SIMBA inaingia sokoni kwa kasi kuimarisha eneo la lango kuelekea msimu wa 2026/27, huku Mwanaspoti likibaini kuwa viongozi wa klabu hiyo tayari wanafanya mazungumzo na makipa watatu tofauti, wakiamini mmoja wao atatua Msimbazi kabla ya dirisha la usajili kufungwa mwezi ujao.


Makipa wanaotajwa kuwa kwenye rada za mabingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB (FA Cup) ni Yona Amosi, Jean Noel wa TRA United na Constantine Malimi wa Mtibwa Sugar.

Taarifa ambazo gazeti hili limezipata zinaeleza kuwa Amosi ndiye anayepewa nafasi kubwa zaidi kutokana na uwezo wake aliouonyesha katika misimu ya hivi karibuni, licha ya kuwa tayari ana mkataba wa Singida Black Stars kwenye gari lake.

Chanzo cha kuaminika ndani ya Simba kililiambia Mwanaspoti kuwa uongozi unaamini bado una nafasi ya kujaribu kumpata kipa huyo kutokana na madai kwamba hajapokea fedha za usajili alizoahidiwa na klabu hiyo iliyomaliza kwenye nafasi nne msimu uliopita wa ligi.

"Tunafahamu Amosi amepewa mkataba na Singida Black Stars, lakini bado kuna mazingira tunayafuatilia, inaelezwa hajapewa fedha zake. Ndiyo maana bado hatujaondoa jina lake kwenye mipango yetu," alisema kigogo huyo.

Amosi alimaliza msimu uliopita akiwa na clean sheets nane, baada yakuwa na clean sheets 11 katika msimu wa 2024/25. Si mara ya kwanza kuhusishwa na Simba, kwani hata msimu uliopita alikuwa kwenye rada za klabu hiyo pamoja na watani wao, Yanga.

Mbali na Amosi, Simba pia inafuatilia kwa karibu uwezekano wa kumsajili Jean Noel kutoka TRA United, ambaye alimaliza msimu uliopita akiwa na clean sheets 13, lakini wakiwa na hofu kubwa kuhusu kanuni ya makipa wa kigeni kwa kuwa huyu wanamtaka kama kipa wa pili, msimu uliopita kanuni ilizuia .

"Jean Noel ni mmoja wa makipa tunaowahitaji. Tunaangalia uwezekano wa kuinunua mkataba wake kutoka TRA United. Tukishindwa, tutahamia kwa Constantine Malimi," kilisema chanzo hicho.

Malimi wa Mtibwa Sugar ndiye chaguo la tatu katika mipango ya Simba baada ya kumaliza msimu akiwa na clean sheets nne.

Wakati huohuo, hatma ya kipa Mahamadou Kassali bado haijaamuliwa, licha ya kumaliza msimu uliopita akiwa na clean sheets 16. Inaelezwa kuwa kocha mkuu Steven Barker ameonyesha nia ya kuendelea kuwa naye kikosini.

Kwa upande mwingine, kipa mzawa Hussein Abel anatarajiwa kuondoka baada ya kutokuwa kwenye mipango ya benchi la ufundi.

Katika hatua nyingine, Barker amewataka wachezaji wote waliosalia kikosini pamoja na nyota wapya waliosajiliwa kuripoti siku ya kwanza ya mazoezi, Julai 18, ili aanze maandalizi akiwa na kikosi kamili.

"Kocha hataki kufanya maamuzi ya mwisho kabla ya kuwaona wachezaji wapya mazoezini. Anataka kulinganisha kiwango chao na wale waliopo kwanza kwa kuwa anahofia kuwa kuna muda mchache sana wa maandalizi ya msimu," kilisisitiza  chanzo hicho.