Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnigeria mambo magumu Azam

Muktasari:

  • Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, umeliambia Mwanaspoti, kuwa Abah ni miongoni mwa nyota waliokuwa katika hatari ya kuachwa kwenye dirisha hili kubwa la usajili, hasa baada ya urejeo wa aliyekuwa winga wa kikosi hicho, Kipre Junior.

UONGOZI wa Azam FC huenda ukaachana na winga wa kikosi hicho Mnigeria, Abel Abah baada ya kutoridhishwa na kiwango chake tangu alipojiunga rasmi na matajiri wa Jiji la Dar es Salaam, Januari 30, 2026, akitokea Klabu ya KF Tirana ya Albania.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa timu hiyo, umeliambia Mwanaspoti, kuwa Abah ni miongoni mwa nyota waliokuwa katika hatari ya kuachwa kwenye dirisha hili kubwa la usajili, hasa baada ya urejeo wa aliyekuwa winga wa kikosi hicho, Kipre Junior.

Kipre aliyeondoka Azam FC msimu 2023-2024, akiwa ameifungia timu hiyo mabao tisa ya Ligi Kuu na kujiunga na MC Algiers ya Algeria, amerejea tena ndani ya kikosi hicho jambo linaloweka nafasi ya Mnigeria huyo shakani kwa msimu wa 2026-2027.

Abah alijiunga na Azam FC mwishoni mwa dirisha dogo la Januari 2026, ili kuongezea nguvu kikosi hicho, akichukua nafasi ya Mtunisia Baraket Hmidi aliyeondoka kwa mkopo na kujiunga na Diyala SC inayoshiriki Ligi Kuu ya Iraq.

Hata hivyo, taarifa ambazo Mwanaspoti imezipata zinaeleza  nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji watakaoachwa ili kutoa nafasi kwa nyota wengine wapya, japo suala lake litakamilika kuanzia wiki ijayo chini ya Kocha Mkuu, Mkongomani Florent Ibenge.

"Suala la mchezaji kuondoka au kubakia itategemea na ripoti ya benchi la ufundi ila ni kweli wapo wengine tutakaoachana nao kama ilivyo utaratibu wa kila msimu unapoisha, kwa sasa tusubirie uamuzi wa mwisho kwanza," kilisema chanzo hicho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ofisa Mtendaji Mkuu Msaidizi wa Azam, Rashid Seif alisema kinachoendelea kwa sasa ni tetesi tu kama ilivyokuwa kawaida ya kila dirisha la usajili linapofunguliwa, ingawa taarifa rasmi zitatolewa na klabu hiyo.

Abah anayecheza winga zote mbili kwa maana ya upande wa kulia na kushoto kwa ufasaha akiwa na miaka 23, alijiunga na KF Tirana Julai 4, 2024, baada ya kuondoka FK Metalac Gornji Milanovac ya Serbia na sasa anaweza kuachana na Azam FC pia.