Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yatua Dar kinyonge, Mashabiki wamuimba Kiiza

Simba yatua Dar kinyonge, Mashabiki wamuimba Kiiza

Muktasari:

  • Kikosi cha Simba kimetua uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere,wakiwa wamepoa baada ya jana kufungwa na Kagera Sugar bao 1-0.

WALIONEKANA ni watu waliochoka, huku sura zao zikiwa na huzuni, unataka kujua ni kina nani hao? Ni mastaa wa Simba baada ya kutua uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

Simba wametua leo mchana, wakitokea Bukoba ambapo walikwenda kucheza na Kagera Sugar na kupoteza kwa bao 1-0, jambo lililowakosesha raha mastaa hao.

Walianza kutoka mmoja mmoja, huku wakiwa hawana raha, mashabiki nao hawakuwa nyuma kuwatania na kulitaja jina la Kiiza.

Tofauti na amshaamsha zilivyozoeleka kwa mashabiki wa uwanja wa ndege kuwashabikia mastaa wa Simba wanapokuwa eneo hilo, asilimia kubwa ni kama walikuwa wanawashangaa, huku wafuasi wa Yanga wakiwa na kicheko.

Mashabiki wa Yanga walisikika wakiuliza Kiiza yupo wapi, lakini Msemaji wa Simba, Ahmed Ally hakusita kuwajibu kuwa wamemuacha kwao.
"Anakuja kufanya nini Dar, kwao si Kagera huko mbona mnateseka hivyo jamani," alisikika Ahmed akiwajibu.

Pamoja na mashabiki wa Yanga, kuonekana kuwapopoa wachezaji wa Simba, lakini kutokana na ustarabu wa Ahmed walimuomba kupiga naye picha.

Baada ya mashabiki hao kumaliza kupiga picha walianza kumwambia Ahmed kwamba aachane na Simba inamkondesha.

"Simba ni timu kubwa, imepitia kicheko na magumu mashabiki wetu ni wavunilivu, muda si mrefu kicheko kinakuja,"amesema.
Mashabiki wa Simba, hawana raha baada ya kufungwa bao 1-0 na Mbeya City, suluhu na Mtibwa Sugar na kuchapwa na Kagera Sugar bao 1-0.