Simba yashusha Mholanzi Dar

Muktasari:

  • Mels mwenye uzoefu wa kufanya skaunti duniani ameshiriki kozi mbalimbali za kazi hiyo ikiwa ni pamoja na zile zilizoendeshwa na mkuu wa skaunti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.

Klabu ya Simba imemteua Mels Daalder raia wa Uholanzi kuwa skauti wake mkuu kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano mingine.

Mels mwenye uzoefu wa kufanya skaunti duniani ameshiriki kozi mbalimbali za kazi hiyo ikiwa ni pamoja na zile zilizoendeshwa na mkuu wa skaunti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.

Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania mara kadhaa, ni shabiki mkubwa wa Simba na pia ni mjuzi wa kufanya uchambuzi (soccer analysis) na ana ujuzi mkubwa wa ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

Moja ya sifa kubwa ya Mels ni kuzungumza lugha mbalimbali duniani ikiwa ni pamoja  anaongea lugha kadhaa ikiwemo, Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani.