Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga wakwepana

WATANI wa jadi Simba na Yanga wamepangwa makundi tofauti katika ratiba ya Ligi ya timu za vijana za klabu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara chini ya umri wa miaka 20 (U-20).

Ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Machi 12 katika viwanja tofauti tofauti huku watani hao wa jadi wakipangwa makundi tofauti.

Simba imepangwa kundi B ambapo itaanza kukata utepe Machi 13 dhidi ya KMC mchezo utakaopigwa katika dimba la Chamazi Jijini Dar es Salaam.

Huku watani zao Yanga wakipangwa kundi A ambapo ataanza kwa kupepetana na Namungo mchezo utakaopigwa uwanja wa Majaliwa Machi 12.

Huku Azam FC akipangwa kundi A akinza kuwakabili Ruvu Shooting katika mchezo wake wa ufunguzi utakaolindima kwenye dimba la Mabatini.

Kundi A lina timu za Yanga, Azam, Coastal Union, Polisi Tanzania, Namungo pamoja na Ruvu Shooting.

Huku kundi B Simba, Tanzania Prisons, Mbeya City, KMC, Mtibwa Sugar pamoja na Ihefu.

Huku C likiwa na timu ya Dodoma Jiji, Mwadui FC, JKT Tanzania, Kagera Sugar, Gwambina pamoja na Biashara United.