Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yakuibali yaishe kwa Morrison

Simba yakuibali yaishe kwa Morrison

Muktasari:

  • Klabu ya Simba imekubali kumsamehe mchezaji wake Bernad Morrison kwa kosa la kutoka kambini bila ruhusa.

Klabu ya Simba imemsamehe nyota wake Bernard Morrison baada ya mchezaji huyo kuomba radhi kwa makosa ya utovu wa nidhamu.

Morrison alisimamishwa tangu Februari 04, 2022 kwa sababu ya utovu wa nidhamu wa kutoroka kambini na uongozi ulimtaka kwenda kujieleza kwenye ofisi ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.
Simba imesema kuanzia sasa mchezaji huyo atarejea kikosini kujiunga na wachezaji wenzake kujiandaa na michezo mbalimbali inayoikabili timu hiyo baada ya kwenda kuomba radhi.
Morrison atakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC ambacho wiki hii kitasafiri kwenda kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi nchini Niger, kisha wataunganisha Moroco kuwafuata RS Berkane.

Mchezaji huyo alikumbana na rungu kama ambalo walilipata nyota wa Azam FC Salum Abubakar 'Sure Boy', Aggrey Morris pamoja na Mudathir Yahya ambao nao walisimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.

Mchezaji huyo amekuwa na kiwango kizuri sana ndani ya Simba kwa mwaka 2021 na ameweza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Juni 2021 akiwashinda Luis Miquissone na John Bocco huku mwezi Novemba 2021 akitwaa tena tuzo hiyo na kuwapiku Jonas Mkude na Meddie Kagere.

Vile vile Morrison alikuwa shujaa kwa mchezo wa kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows baada kuifungia timu yake mabao 2 na kutoa pasi ya bao la tatu kwenye mchezo uliochezwa Novemba 28, 2021 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0.