Simba yaishtaki Al Merrikh CAF

Simba imepeleka  barua rasmi Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuomba uchunguzi kuhusu klabu ya Al Merrikh ya Sudan, kuwachezesha wachezaji wawili waliofungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu la nchini kwao.

Kwa mujibu wa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez amesema  wachezaji hao walifungiwa  katika mchezo namba 93 wa klabu bingwa ya Afrika dhidi yao uliochezwa Machi 6, mwaka huu mjini Khartoum.

Amewataja wachezaji hao kuwa  ni Ramadhan Ajab na Bakhiet Khamis ambao walifungiwa kutojihusisha na michezo kwa miezi sita, kuanzia Junuari 21, 2021 kutokana na kila mmoja kua na mikataba na timu mbili tofauti .

"Tunasubiri kupokea taarifa za uchunguzi kutoka kwa Caf juu ya jambo hili na hatua stahiki zitakazochukuliwa," amesema.