Simba yaifuata Yanga kibabe

RASMI klabu ya Simba imeingia hatua ya nusu fainali ya Kombe la Azam Shirikisho baada ya kuifunga Pamba 4-0 mchezo uliochezwa leo usiku katika uwanja wa Benjamini Mkapa.

Ushindi huo unaifanya Simba ikutane na Yanga ambayo ilishatangulia hatua ya nusu fainaili baada ya kuifunga Geita Gold kwa mikwaju ya penalti.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko Simba ikimtoa John Bocco na kuingia Meddie Kagere wakati huo huo Pamba ilimtoa Salim Juma na kuingia Andrea Mengi.

Dakika 48 Simba ilipata bao kupitia kwa Kibu Denis ambaye alionganisha vizuri krosi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Simba ilipata bao la tatu baada ya Rally Bwalya kupiga krosi na kupita katikati ya mabeki na Yusuph Mhilu aliiunga kwa kichwa na kwenda wavuni.

Dakika 58 John Mbilinyi wa Pamba alifyatuka shuti kali na kutoka nje.

Simba ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Kibu Denis, Mohamed Hussein na Rally Bwalya na kuingia Ousmane Sakho, Gadiel Michael na Sadio Kanoute.

Dakika 60 Malulu Thomas aliingia kwa spidi ndani ya boksi na kupiga pasi lakini mabeki wa Simba waliucheza mpira huo na kipa wa Simba, Beno Kakolanya aliudaka.

Dakika 64 Pamba ilifanya mabadiliko ya kumtoa Robert Mathias na John Mbilinyi kisha waliingia Yusuph Amos na Hassan Salum.

Pamba baada ya kuwa nyuma kwa mabao matatu ilionyesha kujilipua na kucheza kwa kufunguka kwa kushambulia.
 
Dakika 70 ilifanya mabadiliko ya kumtoa Mzamiru Yassin na kuingia Tadeo Lwanga kwenye eneo la kiungo ukabaji.

Dakika 78 Simba ilifanya shambulizi la kushtukiza baada ya Yusuph Mhilu kuchepuka na mpira kwa spidi na kuingia ndani ya boksi alifyatuka shuti kali lakini lilipanguliwa na kipa na kuwa kona isiyokuwa na faida.

Pamba nao walijibu shambulizi baada ya Yusuph Amos kupiga krosi na Hassan Salum aliiunga kwa kichwa lakini kipa Beno Kakolanya aliudaka mpira huo.

Pamba ilifanya mabadiliko mengine akitoka Caleb John na kuingia Moses Nassoro.

Dakika 88 Simba ilipata bao baada ya Gadiel Michael kupiga krosi ya chinichini na kuchezwa na kipa mpira ulienda kwa Yusuph Mhilu ambaye alifyatuka shuti na kwenda wavuni.