Simba yafunga hesabu

Saturday October 09 2021
hesabu pic
By Charles Abel

SIMBA imepiga ndege watatu kwa jiwe moja kabvla ya kuwavaa Jwaneng Galaxy ya Botswana itakayochezwa Oktoba 17.

Kwanza ni kupungua kwa idadi ya majeruhi kutoka saba hadi watatu na hivyo benchi la ufundi sasa lina uhakika wa kutumia . Wachezaji hao ni mabeki Kennedy Juma na Joash Onyango, viungo Sadio Kanoute pamoja na Lwanga Taddeo

Wakati Kanoute aliyeumia katika mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga akiwa yuko fiti na ameshaanza mazoezi, Onyango, Lwanga wao wako kamili na juzi walicheza mechi za timu zao za taifa wakati Nyoni na Kennedy Juma walifanya mazoezi na Taifa Stars na wamekwenda Benin kwa mechi ya marudiano.

“Kennedy yuko vizuri. Jicho lake ambalo ndio ogani kuu ya kuona liko sawa kabisa lakini ile ngozi ya juu ndio imeathirika kidogo lakini haimzuii yeye kuendelea na mazoezi yake,” alifafanua daktari wa Taifa Stars, Lisobine Kisongo

Kitendo cha idadi kubwa ya wachezaji wake kupata nafasi ya kucheza katika vikosi vya timu za taifa, kimesaidia kuwapa ufiti wa hali ya juu wa mechi kabla hawajakabiliana na Jwaneng kulinganisha na wenzao ambao walibakia ambao leo walicheza mchezo wa kirafiki na Cambiasso.

Jambo la tatu ni uhakika wa kuwapata mapema wachezaji wake wengi waliokwenda kuzitumikia timu zao za taifa kutokana na urahisi wa usafiri kutoka maeneo wanakochezea mechi zao.

Advertisement

Mratibu wa Simba, Ali Abbas Seleman alisema; “Wachezaji wengi tutaondoka nao pamoja kwenye msafara wa kwenda Botswana kwani watakuwa wamesharejea,wachache tutaungana nao kule Botswana.” Mwanaspoti linafahamu kwamba Onyango, Lwanga na Medie Kagere wataungana na Simba, Oktoba 11. Lakini pia kutokana na Taifa Stars kwenda Benin na ndege ya kukodi, wachezaji wa Simba wataungana na kikosi chao siku hiyohiyo ya Oktoba 10.

Advertisement