Simba yachomoa kifaa Yanga

Sunday September 19 2021
kifaa pic
By Thomas Ng'itu

MABOSI wa Simba safari hii wamemua baada ya kumchomoa mchua misuli wa Yanga anayefahamika kwa jina la Farid raia wa afrika Kusini.

Farid alionekana katika tamasha la Simba Day na kutambulishwa miongoni mwa viongozi wanaounda benchi la ufundi.

Wakati mechi inataka kuanza Farid pia aliongozana na benchi la ufundi na kwenda kukaa nao pamoja kwenye sehemu yao maalum.

Farid amedumu na Yanga kwa takribani misimu miwili akitoa huduma ya kuchua misuli kwa wachezaji.

Awali upande wa Simba kulikuwa hakuna mchua misuli bali walikuwa na Adel Zrane ambaye yeye ni mtaalamu wa viungo.

Ikumbukwe kuwa Farid alipokuwa Yanga alikuwa na kitanda maalum ambacho alikuwa anatumia kuchua misuli wachezaji.

Advertisement
Advertisement