Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaachana na Zoran

New Content Item (1)
New Content Item (1)

KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya pande zote mbili kwa ajili ya kuachana na kocha wake mkuu Mserbia, Zoran Maki.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kupitia kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo ilieleza kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja aliousaini pamoja na kocha wa viungo, Sbai Karim na kocha wa makipa Mohammed Rachid.

Kikosi hicho ambacho kinajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa tatu dhidi ya KMC kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kitakuwa chini ya Kocha msaidizi Selemani Matola huku mchakato wa kutafuta Kocha Mkuu ukiendelea.

Katika michezo miwili ambayo Zoran alikiongoza kikosi hicho ameshinda yote akianza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold Agosti 17 kisha ushindi wa 2-0 kutoka kwa Kagera Sugar Agosti 20 yote ikichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Zoran mwenye uraia pacha wa Serbia na Ureno alitambulishwa rasmi kukinoa kikosi hicho Juni 28 mwaka huu akichukua mikoba ya Mhispania Pablo Franco aliyejiunga nayo Novemba 10, 2021 kabla ya kutimuliwa Mei 31, 2022.