Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba ya Fadlu yamkosha Azim Dewji

Fadlu Pict

Muktasari:

  • Dewji katika mechi mbili za hivi karibuni ambazo Simba imeenda kucheza ugenini dhidi ya CS Sfaxien (Tunisia) na Bravos (Angola), amesafiri na kikosi hicho kilichokusanya pointi nne baada ya kushinda 1-0 na sare ya 1-1.

SIMBA imerudi nchini ikiwa na tiketi yake mkononi ya kucheza robo fainali ya sita kwenye mashindano ya Caf na kwenye msafara wa timu hiyo alikuwemo mfadhili wao wa zamani, Azim Dewji, ambaye ameshuka na maneno mazito juu ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Fadlu Davids.

Dewji katika mechi mbili za hivi karibuni ambazo Simba imeenda kucheza ugenini dhidi ya CS Sfaxien (Tunisia) na Bravos (Angola), amesafiri na kikosi hicho kilichokusanya pointi nne baada ya kushinda 1-0 na sare ya 1-1.

Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kuwasili kwa kikosi hicho kikitokea Angola, Dewji alisema amekoshwa na namna uongozi wa Bodi ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Mohammed Dewji akisema hatua ya kwanza ya kukisuka kikosi hicho imefanyika kwa kiwango kikubwa.

Alisema, ameridhishwa na ubora wa wachezaji ambao wamesimama imara kwenye mechi za ugenini na hata za nyumbani huku akisema Simba ina nafasi ya kuongoza hata kundi lao.

“Kwanza niipongeze Bodi ya Wakurugenzi ya Simba chini ya Mohammed (Dewji), unajua mimi sijasafiri na Simba kwa takribani miaka 32, tangu niliposimama kuifadhili lakini hizi mechi mbili za ugenini nikasema acha niende nikaone timu inachezaje kwa macho yangu,” alisema Dewji na kuongeza.

“Nilikuwa Tunisia na nikaenda Angola, msingi wa safari hizi mbili ni maagizo ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan alitaka niende kuhamasisha timu ipate mafanikio na ifuzu, namshukuru Mungu yote  yamewezekana lakini pia  nimeridhishwa na ubora wa kikosi chetu, hii ndio Simba ambayo mashabiki walikuwa wanaililia

“Unaona namna wachezaji wanacheza kwa ubora hasa hizi mechi za ugenini hata ile mechi ambayo tulipoteza ilikuwa ni makosa yetu na baada ya hapo vijana wakabadilika, kwa namna nilivyoiona Simba kule na tunarudi nyumbani tuna uwezo kabisa wa kumaliza kinara wa kundi letu sina Mashaka hata kidogo.

“Hamasa ya soka sasa ni kubwa, nimeona hata Rais Samia Suluhu Hassan anavyoongeza hamasa kwa wachezaji wetu, ukiwa ugenini mabalozi wako karibu na timu utasema ni timu ya Taifa, hii inaongeza utulivu kwa timu.

“Benchi la ufundi nalo lipo imara sana huyu kocha Fadlu (Davids) ameonyesha akili kubwa anavyocheza hizi mechi, nadhani kama tukimaliza kinara wa kundi tunaweza kwenda kucheza nusu fainali au hata fainali ya mashindano haya ya Shirikisho.”

Wikiendi hii Simba itaikaribisha CS Constantine kutoka Algeria katika mchezo wa mwisho Kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Endapo Simba itashinda, itamaliza kinara wa kundi hilo ambalo sasa linaongozwa na Constantine yenye pointi 12, wakati Simba inazo 10.