Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba wamalizana na kiungo Mcongo

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Baada ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 15 ,  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa orodha ya wachezaji wote waliosajiliwa na klabu mbalimbali hapa nchini.

Katika usajili huo kumekuwa na sapraizi kwa klabu ya Simba ambao katika wachezaji wao wawili waliosajiliwa kwa ajili ya Ligi Kuu na michuano mingine limekuwepo jina la nahodha wa DC Motema Pembe, Doxa Gikanji.

Usajili huo umezua gumzo kutokana na kutokuwepo tetesi za awali za ujio wake kama ilivyo kwa nyota wengine wa klabu kubwa za Azam, Yanga na Simba.

Gikanji mwenye miaka 30 anayemudu nafasi ya kiungo mkabaji kwa sasa yupo na timu ya DR Congo nchini Cameroon kwenye michuano ya Chan na atajiunga na Simba pindi itakapomalizika michuano hiyo.

Simba imesajili wachezaji wawili katika dirisha dogo na kuleta maswali kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao wanahoji kwa nini jina la kiungo Mganda,  Taddeo Lwanga halipo na wakati  tayari walishatangaza kumsajili na walimtambulisha Desemba 2 mwaka jana.


Gazeti la Mwanaspoti kesho Januari 22, 2020 litakuja na majibu yote ya sakata la usajili wa Simba, usikose nakala yako.