Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba waja na ‘Total War’ kuwamaliza Al Ahly

New Content Item (1)
New Content Item (1)

BAADA ya kauli mbiu ya ‘War in Dar’ kufanikiwa kuwaongoza Simba kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya FC Platnum ya Zimbabwe na kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, leo hii wamekuja na ‘Tatal War’ kwaajili ya kuwakabili Al Ahly Jumanne 23 kwenye dimba la Benjamin Mkapa.

Hayo yamesemwa leo na Ofisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo amesisitiza kuwa kauli mbiu hiyo itumike ili kuwapa nguvu wanasimba wote kuelekea mchezo huo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Haikuishia hapo, Manara pia kwa niaba ya Simba wameongezea maneno kwenye kauli mbiu hiyo ya ‘Point of no return’ yenye maana ya hatua ya kutorudi nyuma hivyo msemo huo kwa ujumla ni Tatal War ‘Point of no return’.

“Hii ni sawa na mtu kuwa porini halafu akutane na Chui, lazima apambane bila kukata tamaa vinginevyo atauliwa, hiyo ndio maana halisi ya kauli mbiu yetu hiyo ambayo itawafanya wachezaji waingie uwanjani wakiamini kuwa hakuna nafasi nyingine zaidi ya kushinda,” amesema Manara.

Hivi karibuni Simba kupitia kwa Ofisa wao Manara wamekuwa wakitoa kauli mbiu ambazo wanaamini zinasaidia kupata ushindi na miongoni mwa kauli mbiu hizo ni Tiki taka kwa Mkapa, War in Dar na hii ya sasa ya Total War ‘Point of no return’.

Mchezo wa Simba dhidi ya Ahly utakua wapili kwao kwenye michuano hiyo hatua ya makundi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini DR Congo dhidi ya AS Vita.