Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba vs Dodoma Jiji yabadilishiwa tena muda

Simba vs Dodoma Jiji yabadilishiwa tena muda

Muktasari:

  • MCHEZO wa Ligi Kuu ya NBC kati ya wenyeji Simba dhidi ya Dodoma Jiji, uliokuwa uchezwe majira ya Saa 10 Alasiri, sasa umerudishwa kwenye muda wake.

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inawataarifu wadau wote wa Ligi Kuu ya NBC kuwa muda wa kuanza kwa michezo ya Ligi itakayochezwa Jumatatu Machi 7, 2022 imerejea kuwa kama ilivyoainishwa kwenye ratiba ya Ligi iliyotangazwa mwanzoni mwa msimu.

Mchezo namba 132, Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji FC utachezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku kama ilivyo kwenye ratiba ya Ligi badala ya saa 10:00 alasiri iliyotangazwa leo.

Mchezo namba 136, KMC FC dhidi ya Coastal Union FC utachezwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 10:00 alasiri kama ilivyo kwenye ratiba ya Ligi badala ya saa 1:00 usiku iliyotangazwa leo.

Mabadiliko ya muda wa kuanza michezo yaliyotangazwa leo yalitokana na taarifa ya mmiliki wa uwanja wa Benjamin Mkapa kuhusu nia yake ya kuifanyia huduma kinga (service) ya kawaida kangavuke (Generator) ya uwanja huo.

Hata hivyo, kutokana na jitihada zilizofanyika, zoezi hilo litakamilika mapema na kuruhusu kangavuke hiyo kutumika kwa mchezo wa Simba dhidi ya Dodoma Jiji.