Simba SC mechi mbili siku moja

Turan PFK
Simba SC leo Julai 27 itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Turan PFK inayoshiriki Ligi Kuu Azerbaijan.
Mechi ya kwanza itapigwa saa 5 asubuhi na ya pili saa 12 jioni ambapo Simba imesema lengo ni kila mchezaji kupata muda wa mrefu wa kucheza.
Timu hiyo imepiga kambi Ankara nchini Uturuki sawa na Simba ilishika nafasi ya sita msimu ulioisha tayari imecheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Adana na Eyupspor waliyoifunga mabao 2-1.
Simba imecheza mechi moja tayari dhidi ya Zira FC iliyomalizika kwa kufungana bao 1-1.
Simba inatarajiwa kutua nchini Agosti Mosi kujiandaa na tamasha la Simba Day itakapocheza dhidi ya Power Dynamos ya Zambia Agosti 6.