Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Queens yaambulia sare, kuikabili Kenya Police Bullets

Muktasari:

  • Licha ya matokeo hayo tayari, Simba ilishafuzu nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ethiopia, baada ya kushinda michezo miwili ya awali ya Kundi B.

Wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya timu za soka za wanawakw ukanda wa Cecafa, Simba Queens wamemaliza kibabe mechi za makundi kwa kulazaimishwa sare ya 2-2 dhidi ya PVP Buyenzi ya Burundi.

Licha ya matokeo hayo tayari, Simba ilishafuzu nusu fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Ethiopia, baada ya kushinda michezo miwili ya awali ya Kundi B.

Simba imemaliza ikiwa pointi saba sawa na Kawempe Muslim Ladies ya Uganda inayoshika nafasi ya pili.

Katika nusu fainali Simba itacheza na Kenya Police Bullets, huku Kawempe Muslim Ladies ikikutana na wenyeji CBE ya Ethiopia. Bingwa wa michuano hiyo atafuzu Klabu Bingwa Afrika.