Simba, Namungo zagawana pointi

BAO la kusawazisha la mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke limeihakikishia timu hiyo pointi moja baada ya kutoka sare ya 1-1 na Namungo FC kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.

Baleke ameendeleza rekodi nzuri kwani hata mchezo wa mwisho waliotoka sare kama hiyo alifunga bao katika Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza ziliwaondoa Simba vichwa chini baada ya bao ya Namungo kupata bao dakika ya 29 likifungwa na Reliants Lusajo lililowafanya mashabiki kupiga kelele muda wote.

Kipindi hicho timu zote zilishambuliana zamu kwa zamu lakini mashambulizi ya Simba hayakuzaa matunda chini ya mikono salama ya mlinda mlango wa Namungo, Jonathan Nahimana.

Hata Namungo walifanya mashambulizi ya kushtukiza yakadhibitiwa vyema na Ayoub aliyekuwa langoni kwa upande wa Simba hii leo.

Kipindi cha pili mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa wekundu hao yaliongeza chachu ya mapambano kwa timu yao kuonyesha uhai.

Mabadiliko hayo yalikuwa hivi alitoka Onana na kuingia Moses Phiri, Saido akaingia Shaban Chilunda, akatoka Chama na kuingia Luis Miquissone, Fabrice Ngoma akaingia John Bocco, pia akatoka Che Malone na kuingia Kennedy Juma.

Huku Namungo alitoka Lusajo na kuingia Kelvine Sabato, Domayo na kuingia Shiza Kichuya, Buswita akatoka na kuingia Blandja.


REKODI YAO

Katika michezo nane ambayo walikutana kabla ya huu wa leo Simba ilishinda mitano na kutoka sare mitatu.

Januari 29/2020 Simba 3-2 Namungo, Julai 8/2020 Namungo 0-0 Simba, Mei 29/2021 Namungo 1-3 Simba, Julai 18/2021 Simba 4-0 Namungo, Novemba 3/2021 Simba 1-0 Namungo, Mei 3/2022 Namungo 2-2 Simba, Novemba 16/2022 Simba 1-0 Namungo, Mei 3/2023 Namungo 1-1 Simba.

Hata hivyo huu ni mchezo wa tatu kuongozwa na kocha Denis Kitambi baada ya kuchukua nafasi ya Cedrick Kaze aliyefungashiwa vilago hivi karibu.

Katika michezo miwili ameshinda mabao 3-1 dhidi ya Azam FC huku akiambulia sare ya bila kufungana na Coastal Union.

Kaze yeye aliiongoza Namungo michezo sita akiambulia sare tatu na kupoteza tatu hakufanikiwa kunusa ushindi wowote ule.

Wachezaji wa Simba walioanza katika mchezo wa leo Ayub, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Malone Fondoh, Henock Inonga, Mzamiru Yassin, Fabrice Ngoma, Jean Baleke, Saido Ntibazonkiza na Willy Onana.

Namungo walianza Jonathan Nahimana, Hassan Kibailo, Emmanuel Asante, Derrick Mukombozi, Erasto Nyoni, Hamis Nyenye, Hashim Manyanya, Frank Domayo, Reliant Lusajo, Pius Buswita na Jacob Masawe