Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba marufuku kumzingua Kichuya

Muktasari:

  • Kichuya ndiye kinara wa mabao ndani ya Simba tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu uliopita ambapo amefunga mabao 15 ya Ligi Kuu Bara

NAHODHA wa zamani wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ amefichua mambo yanayowabeba nyota wawili wa Simba, Mzamiru Yassin na Shiza Kichuya ambao wamejiapambanua kuwa mastaa wakubwa klabuni hapo.

Hata kocha, Joseph Omog, amepewa maelekezo jinsi ya kuwapandisha mzuka wachezaji hao.

Kichuya ndiye kinara wa mabao ndani ya Simba tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu uliopita ambapo amefunga mabao 15 ya Ligi Kuu Bara akifuatiwa na Ibrahim Ajibu mwenye mabao tisa. Lakini Ajibu amehamia Yanga.

Mzamiru amekuwa nyota muhimu ndani ya Simba na kikosi cha Taifa Stars ambapo msimu uliopita alifunga mabao manane Ligi Kuu licha ya kucheza nafasi ya kiungo.

“Ni wachezaji wenye nidhamu kubwa, muda mwingi wananipigia simu na kuomba ushauri. Tangu msimu uliopita wamekuwa wakisikiliza ushauri na kujifunza, pamoja na Mavugo (Laudit). Wanajituma sana,” alisema Mgosi.

“Kichuya amekuwa mchezaji mwenye kitu cha ziada pia. Anajitahidi kufunga japo sio kazi yake ya msingi. Kazi yake kubwa ni kutengeneza nafasi, lakini amekuwa na jicho la goli.

“Niwaambie mashabiki wa Simba kuwa siku ikitokea Kichuya hajafunga tusimhukumu. Kufunga si jukumu lake.”

Lakini pamoja na Mzamiru na Kichuya, kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni, ameuangalia mwenendo wa timu hiyo na akawashauri wachezaji wawe waadilifu wasilewe sifa.

“Kwanza niwapongeze kwa ushindi dhidi ya Stand United, lakini lazima watathimini changamoto waliyoiona, hilo litawaongezea umakini,”alisema.

Kibadeni pia alilishauri benchi la ufundi kuwajenga wachezaji ili wasitoke kwenye ari ya mchezo.