Simba kukipiga na Warundi

Tuesday September 14 2021
aigle pic
By Waandishi Wetu

Simba iko kambini Arusha ikiajiandaa na michuano mbalimbali inayowakabili ikiwemo Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga Septemba 25.

Leo timu hiyo itacheza mechi ya tano ya kirafiki dhidi ya Aigle Noir ya Burundi ingawa awali ilicheza mechi zingine zikiwemo walipokuwa Morocco.

“Naendelea na maandalizi kwa ajili ya kikosi. Wachezaji wako vizuri na kambi imetulia, nina imani malengo yetu yatatimia kama ilivyokuwa msimu uliopita, “ alisema kocha Gomes, ambaye timu yake itaivaa TP Mazembe ya DR Congo katika mechi ya kirafiki kwenye Tamasha la Simba Day Jumapili hii.

Wakati Simba walikuwa Morocco kujiandaa na msimu mpya, Mazembe pia walikuwa nchini humo ambako walicheza mechi tatu za kirafiki na kuambulia ushindi mara moja dhidi ya Club Chabab Riad Salim wa bao 1-0, suluhu na Wydad Casablanca na kupoteza kwa kufungwa 2-1 na Sporting Club Chabab.

Maandalizi hayo yanaonyesha mechi ya Simba Day itakuwa kipimo kizuri kwa Simba inayojiandaa kuivaa Yanga.

Advertisement