Simba, Kaizer Chiefs kitaeleweka Jumamosi hii

Simba
Simba

Muktasari:

Baada ya sekeseke la mechi ya watani wa jadi (Simba na Yanga) iliyokuwa ipigwe Jumamosi iliyopita kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam kuwaacha wapenda soka vinywa wazi, utamu umehamia ligi ya mabingwa Afrika ambapo mnyama (Simba) Jumamosi atakuwa dimbani jijini Johannesburg kuminyana na wenyeji wao Kaizer Chiefs.

Hii ni mechi ya kwanza ya hatua ya robo faina ya ligi ya mabingwa Afrika ambayo timu hizi zilimaliza nafasi ya kwanza na ya pili kwenye makundi hayo.

Simba ikiwa na kikosi kamili imetua kwa madiba kwa lengo la kupata ushindi kwenye mchezo huo huku wenyeji wao wakijidhatiti kumsimamisha mnyama ambaye msimu huu ameonekana kuwa tishio kwa vigogo wengi wa Afrika.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii, Mei 15 katika dimba la FNB jijini Johannesburg Afrika Kusini kuanzia majira ya saa kumi na mbili jioni kwa saa za Afrika Kusini na saa moja kamili jioni kwa saa za Tanzania.

Unaweza kutazama mechi hii kupitia KBC 1 chaneli namba 270 kwenye kisimbuzi cha DStv pekee. Usikose.