Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Kagera hakuna kisingizio, Chama aongeza mzuka

MAKOCHA wa Simba na Kagera wamekiri kwa midomo yao kwenye mechi ya leo hakuna kisingizio chochote lazima kipigwe na mtu aondoke na pointi.

Hakuna cha hali ya hewa, ugonjwa wala miundombinu kinachotakiwa ni pointi tatu. Awali mechi hiyo iliahirishwa mwezi Desemba mwaka jana baada ya Simba kutoa utetezi wachezaji wao zaidi ya 10 waliugua mafua.

Kocha wa Simba, Pablo Franco ameliambia Mwanaspoti kiuhalisi kwa mabadiliko ya kiufundi wanayokwenda kuyafanya dhidi ya Kagera pamoja na rekodi hategemei kukosa ushindi na bado anaamini timu yake ipo kwenye mbio za ubingwa kwani ligi bado mbichi.

“Tunapaswa kushinda mchezo huu bila kisingizio chochote kwa vile matokeo ya mechi mbili zilizopita hatukuwa vizuri na bado mnapaswa kuelewa Simba ipo kwenye mbio za ubingwa,” alisema Pablo.

Aliongeza kuna mbinu na mabadiliko kadhaa ya kiufundi kwenye safu ya ushambuliaji ambayo anaamini yanakwenda kuwapa matokeo kwenye mechi hiyo ngumu.

“Kikosi chetu kinatengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao katika kila mechi ila kuna shida kidogo, tutafanyia kazi katika uwanja wa mazoezi na naamini wakifanya vizuri huku watatengeneza hali ya kujiamini na kufanya kama hivyo kwenye mechi.”

Kocha John Baraza wa Kagera alisisitiza kwa hali waliyonayo kwenye msimamo wa ligi hawana chochote cha kueleza zaidi ya ushindi huku straika wake mkongwe, Hamis Kiiza akiahidi ushindi.

“Ni mchezo mgumu lakini nitatumia uzoefu wangu na wachezaji wenzangu kupata matokeo, tuache miguu izungumze,” alisema Kiiza aliyewahi kucheza Simba na Yanga.

Hata hivyo Baraza hadi jana alikuwa hajajua hatma ya nyota wake watatu Hassan Mwaterema, Said Kipau na David Luhende huku akisema walipata majeruhi kwenye mchezo wa Dodoma Jiji walioshinda mabao 2-1, mabao yote yalifungwa na Mwaterema.

“Walipata mshituko kidogo hali iliyowapelekea kuwa na maumivu makali, nasubiri hadi kesho asubuhi(leo), ndio nitajua kama watakuwa sehemu ya mchezo au laah! ingawa nina matumaini makubwa watakuwa fiti kwa sababu ni wachezaji muhimu kwenye kikosi changu na ninawategemea,” alisema.


REKODI ZAO

Rekodi mbovu ya Kagera Sugar katika mechi 10 za hivi karibuni kwenye uwanja wao wa nyumbani inaweza kuwabeba Simba leo inapoikabili timu hiyo kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba.

Katika mechi 10 zilizopita za Ligi Kuu Bara tangu April mwaka jana, Kagera imeshinda mechi tatu tu huku ikipoteza tano na kutoka sare mbili wakati Simba katika mechi 10 za ugenini tangu Juni mwaka jana, imeshinda sita, imetoka sare mitatu na kupoteza mmoja tu dhidi ya Mbeya City.

Pia katika mechi tano zilizopita ambazo Kagera na Simba zimekutana kwenye uwanja huo, wekundu wa Msimbazi wameshinda tatu wakati wenyeji wameshinda mbili.

Mara ya mwisho Kagera Sugar kuifunga Simba kwenye uwanja wa Kaitaba ni Aprili 19, 2019 waliposhinda mabao 2-1 lakini mechi nyingine mbili zilizofuata zote walipoteza.

Aprili 21 mwaka jana, Simba iliichapa Kagera mabao 2-0, Septemba 29, 2020 Kagera ilifungwa na Simba mabao 3-0, Aprili 19, 2019 Kagera iliifunga Simba mabao 2-1 wakati Januari 22, 2018 Simba iliibamiza Kagera mabao 2-0 huku April 2, 2017. Kagera iliiadhibi Simba mabao 2-1.

Hata hivyo, Simba itaingia katika mchezo wa leo ikiwa katika presha kubwa ya kusaka matokeo mazuri ili kurejesha furaha kwa mashabiki wake ambao hawaelewi nini kimeikumba timu yao.

Kama Simba itapoteza mchezo wa leo, hali inaweza kuwa mbaya zaidi katika klabu hiyo kwani wameachwa na watani zao wa Jadi Yanga pointi 10.

Jambo ambalo linawaumiza mashabiki ni jinsi mastraika wao tegemeo, Meddie Kagere, John Bocco na Chriss Mugalu waliokuwa vinara wa ufungaji msimu uliopita kushindwa kufunga katika mechi tano mfululizo za ligi na tayari kocha wa Kagera Sugar, Francis Baraza amewapangia mkakati wa kuwadhibiti kifundi.

KWA MAONI KUHUSU HABARI HII TUANDIKIE: 0658376417