Shujaa Kids kuhamasisha michezo kwa watoto

Katika kuhamasisha michezo kwa watoto Shujaa Dyanamic Wellness and Fitness Activation Dynamic imeandaa tamasha kubwa likiitwa Shujaa Kids Temple Run.

Tamasha hilo limehamasishwa na michezo (mbio) linazinduliwa tarehe 9 Disemba 2023 katika ukumbi wa Police Officer Mess huko Masaki kuanzia saa 2:00 asubuhi.

Akizungumzia tamasha hilo, Ofisa Habari wa Shujaa Dynamic, Catherine Mbaga amesema licha ya mbio hizo kutakuwa na michezo mingine kama kuendesha farasi, kuteleza, bembea za Zipline na Kuruka vikwazo.

“Washiriki watafanya kazi pamoja kama timu ili kushinda vikwazo vilivyowekwa vilivyotokana na mchezo huku wakifungua mafumbo ya gemu.”

Kwa miaka miwili sasa Shujaa Dynamic hiyo imekuwa ikiandaa  michezo na matukio makubwa manne “Shujaa Kids camps”  na ya kiasi zaidi ya 20  ambayo yalifanyika kwa ufanisi mkubwa yakiwemo ya wikiendi yaani “Shujaa Kids school training” ambayo mara nyingi hufanywa kila wikendi Jumamosi asubuhi.

Kupitia shughuli zake imesaidia kukuza afya na akili za watoto na wazazi.  Watoto wanaoshikiriki huwa shupavu huku ikifundisha stadi muhimu za maisha kama vile kutatua matatizo, kazi ya pamoja na ustahimilivu.