Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sherehe ya mke wa Tambwe imedamshi kwa sapraiz kibao

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe alikamilisha taratibu za kumwoa  mwanamke aliyeishi naye kwa takribani miaka mitano anayeitwa Raiyan. Tambwe na Raiyan wamefanikiwa kuzaa mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Ayman.

KWA taarifa yako tu, juzi Jumamosi mke wa straika wa kimataifa wa Yanga, Amissi Tambwe, Raiyan alifanyiwa sherehe kupongezwa kwa kufunga ndoa na nyota huyo kutoka Burundi.

Sasa unaambiwa kwenye sherehe hiyo, wake wa nyota mbalimbali wa soka nchini walidamshi kinoma kwa jinsi walivyofanya kufuru kumpongeza mwenzao kwa kuachana na kambi ya makapera na kuingia kwenye kambi ya wanandoa.

Ni hivi, umoja wa wanawake wa nyota wa soka nchini, waliamua kufanya bab’kubwa kwa kumzawadia mwenzao, Raiyan kiwanja, huku mke wa Kelvin Yondani, Nance Mussa akimwaga noti kama pedejee fulani hivi.

Tukio hilo ambalo liliweka gumzo maeneo ya Ilala katika Ukumbi wa CCM Ilala Boma ukiwa ni mwendelezo wa sherehe za kusindikiza ndoa yao. Walianza na singo (Kitchen Party), ikaja ndoa na hiyo ya usiku wa zawadi na sasa wanajiandaa na sherehe nyingine kubwa itakayofanyika Burundi nyumbani kwa kina Tambwe.

Msemaji wa umoja huo ambao unajulikana kwa jina la Thamani ya Mwanamke, Ummy Carlos alimkabidhi hati hiyo ya kiwanja ambacho kipo maeneo ya Kibamba chenye ukubwa wa mita 40 kwa 50 chenye thamani ya Sh 1.3 milioni.

“Sisi wanakamati ya maandalizi tumeona kiwanja hiki ni zawadi na ukumbusho mkubwa kwake,” alisema Ummy.

Mbali na mke wa Yondani, baadhi ya waliokuwepo ni mke wa Beno Kakolanya (Hadra), Geofrey Taita (Ashama), Ibrahim Ajibu (Amina) sambamba na wake wa kadhaa wa nyota soka kama wa Ally Shomary, Ibrahim Job, Kelvin Sabato, Jackson Chove, Abdallah Seseme na Said Ndemla.

MKE WA YONDANI

Kwa upande wa mke wa Yondani, mbali na zawadi hiyo ya jumla, alionyesha jeuri ya pesa na kwenda kumtunza ya kwake na kutoa kiasi cha shilingi laki moja.

“Tumekuwa karibu nikaamua kufanya hivyo kwa sababu ya uhusiano wetu,” alisema Nance ambaye pia walifunga ndoa na Yondani mwaka jana lakini wamekuwa wakiishi pamoja kwa zaidi ya miaka 10.

RAIYAN AMWAGA CHOZI

Katika hali isiyotarajiwa, mke wa Tambwe alishindwa kuvumilia na kudondosha machozi wakati akifanya utambulisho kwa ndugu zake.

Raiyan ambaye amezaa na Tambwe mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Ayman alilia alipokuwa anawatambulisha dada na ndugu wa Tambwe waliofunga safari kutoka Burundi hadi Dar kwa sababu ya tukio hilo.

“Unajua imetokea tu nikalia, kingine nilikuwa nawaza naenda mbali, Burundi, nawaacha wazazi na watu niliowazoea,” alifafanua Raiyan.

NDUGU WA TAMBWE NOMA

Dada na ndugu wa Tambwe walifanya kituko wakati wa kutoa zawadi kwani waliingia ukumbini na begi lililokuwa limejaa vitenge na khanga za Burundi ambazo walizitoa kwa madoido moja moja wakimtunza wifi yao.

TAMBWE AINGIA MITINI

Sherehe hizo ambazo zilihudhuriwa na wanawake tu na wanaume wachache waliokuwepo ukumbini hapo kwa sababu ya kuwa na kazi maalumu kama ilivyofanywa Mombasa wakati msanii Ali Kiba alipochukua jiko. Hadi mwisho Tambwe hakutokea ndani ya ukumbi kwa madai hilo lilikuwa ni tukio la wanawake. Pia, katika usiku huo, wanawake hao walionyeshana ubabe wa Usimba na Yanga.

ALICHOSEMA MKE WA TAMBWE

“Nashukuru kwa yote tumemaliza hili na sasa tunajipanga kwa ajili ya sherehe ya Burundi. Nashukuru Tambwe kwa kunipa heshima hii ya kuwa mkewe,” alisema Raiyan ambaye MC wake alikuwa ni mke wa mwimbaji wa muziki wa Singeli, Msaga Sumu.