Sherehe Mkwakwani zimeanza mdogo mdogo

NJE ya Uwanja wa Mkwakwani uliopo Tanga, hali ya mashabiki sio kubwa ingawa bado wanaendelea kuja, kuzishuhudia mechi ya Coastal Union dhidi ya Simba zikicheza jioni, mechi ya Ligi Kuu Bara.

Kuna mashabiki wametulia kwenye baa, migahawa ya chakula, huku wengine wakikatiza mitaa barabara ya Mkwakwani, ya nne na tatu.

Asilia ya rangi zilizovaliwa ni jezi nyekundu , nyeupe zilizo na wekundu na kijani na njano.

Uwepo wa mashabiki hao, baadhi ya wafanya biashara ambao wanauza dagaa uono (dagaa nyama), mahindi, supu za samaki na nyama ya ng'ombe, mahindi ya kuchemsha, wameeleza namna wanavyofaidika na mechi hiyo kibiashara.

Mfanyabiashara mdogo mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Mariam Rashid anauza dagaa uono, amesema kucheza Coastal Union na Simba anapata faida ya biashara yake, kutokana na uwingi wa mashabiki.

"Biashara ni watu zinapokuja kucheza Simba na Yanga hapa kwetu ni raha, si umeona hawa dagaa uono wapo wa kuchemsha na kulosti watu wa nje na Tanga wanapenda," amesema Maria.

Pembeni yake yupo  kaka anayeuza mahindi ya kuchemsha, amejitambulisha kwa jina la Mohamed Habibu amesema leo anatarajia kupiga pesa ndefu, kutokana na mashabiki watakaokuwepo.

Wakati huohuo biashara za jezi za Simba na Yanga zinaendelea ingawa hazikuonekana za Coastal Union ambao ni wenyeji wa mchezo huo.