Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serena hafikiri kustaafu kucheza tenisi

Muktasari:

Serena akiwa na miaka 37 hivi sasa haionekani kuwa tayari kustaafu tenisi wakati wowote hivi karibuni.

Marekani. Serena Williams asema hayuko tayari kustaafu kucheza tenisi hivi karibuni baada ya kuitumikia kwa miaka 20 sasa.

Serena mwenye miaka 37, amesema hayo jijini New York wakati alipohudhuria jopo la ‘Advertising Week New York’ kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Verizon, Guru Gowrappan na mwandishi wa CNBC, Julia Boorstin.

Alipoulizwa kuhusu kustaafu kwake Serena alisema "Nasikirilii kustaafu, unajua ndani ya miaka 20, sio muda mrefu," kisha wote wakacheka.

Wakijadiliana na mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya Verizon Media Group ambayo ni  kampuni yake ya mavazi na kampuni ya ubia.

Akiwa pia ni mwanzilishi wa kampuni ya ubia, inayoitwa Serena Ventures aliongea juu ya uwekezaji, "Napenda teknolojia hata hivyo, waanzilishi wanawazingatia sana wawekezaji wa kike" alisema Serena.

 

 

Alizungumzia mavazi yake ya ‘S by Serena Williams’ na kusema "ukivaa mavazi yetu yanakubadilisha jinsi unavyohisi, unataka kujisikia mwenye mvuto, unataka kujisikia ujasiri na unataka kuhisi hakika ndani yako."

Serena ni mke wa Reddit Alexis Ohanian na mama wa binti wa miaka miwili, Alexis Olympia Ohanian.

Akiadhimisha kuzaliwa kwa mwanaye Septemba 1, Serena kupitia Instagram aliandika “Miaka miwili iliyopita imekuwa ya mafanikio makubwa sana kwangu”.

Kwa tamko alilolitoa mbele ya jopo, Serena akiwa na miaka 37 hivi sasa haionekani kuwa tayari kustaafu tenisi wakati wowote hivi karibuni.